Na Lorietha Laurence
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amefungua rasmi mkutano wa 30 wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki chini ya udhamini wa Benki ya PTA leo jijini Dar es Salaam.
.jpg)
Mhe. Pinda amewasihi washiriki wa mkutano huo wasiishie tu kushiriki katika mkutano bali pia wapatapo nafasi waweze kutembelea sehemu mbalimbali nchini ikiwenmo mbuga za wanayama na vivutio vingine kwa kuwa Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana katika sekta ya Utalii.
“kwa niaba ya Serikali ya Tanzania nimefurahi sana kwa kutupatia nafasi hii ya kuwa wenyenji wa mkutano huu hivyo tunawakaribisha washiriki waweze kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo nchini kwetu pale wapatapo nafasi” alisema Mhe.Pinda

Aliongeza kusema benki ya PTA imesaidia katika kukuza na kuinua uchumi wa Afrika kwa nchi washiriki na kwa kufanya hivyo imeongeza chachu ya kuwepo mshikamano na mahusiano mazuri baina ya nchi hizo.
Aidha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uratibu na Uhusiano Mhe.Steven Wassira kwa niaba ya Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya ameshukur kwa fursa ya kusimamia mkutano huo wenye lengo la kujadili mambo ya kibenki na uchumi kwa nchi washiriki.

“kupitia mkutano huu Tanzania inapata fursa ya kuweza kujadili mambo mbalimbali yanahusu maendeleo na namna ya kujikwamua kutoka katika umaskini tunaishukuru Benki ya PTA kwa kutupa nafasi hii na tunawakaribisha tena kwa wakati mwingine”alisema Mhe. Wassira.
Naye Rais na Mtendaji Mkuu wa Benki ya PTA, Admassu Tadesse ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
Benki ya PTA inatoa huduma zake kwa nchi wanachama ikiwa na lengo la kuwa Taasisi ya kifedha inayoongoza Mashariki na Kusini mwa Afrika katika utoaji wa huduma za kibenki ambapo mwaka huu imetimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1985.


No comments:
Post a Comment