Habari za Punde

*AZAM FC TOLEWA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA, YACHAPWA 3-0

TIMU ya Azam Fc, jana usiku imeungana na wenzao wa KMKM ya Zanzibar kuaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kukubari kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan na hivyo kutolewa kwa jumla a mabao 3-2.
Azam walienda Sudan wakiwa na hazina ya mabao 2-0 iliyopata katika mechi ya raundi ya kwanza wiki mbili zilizopita, kwenye uwanja wake wa nyumbani Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo jana wenyeji walitumia nafasi ya kucheza nyumbani na kubadili matokea kama kocha wao alivyoatamba mapema kabla ya mchezo na Azam kuaga mashindano. 
El Merreikh walikosa pia penati baada ya kupaisha.
Hii ni mara ya pili kwa Azam kuaga michuano ya Kimataifa katika raundi ya awali baada ya mwaka jana pia kutolewa na timu ya Ferroviaro de Beira ya Msumbiji.

Azam imetoka ikiwa ni saa chache baada ya KMKM ya Zanzibar nayo licha ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya El Hilal ya Sudan, ilijikuta ikiaga mashindano hayo kwa ujumla ya mabao 2-1 baada ya mechi ya kwanza nchini Sudan kulala mabao 2-0.

Timu ya Polisi Zanzibar waliokandamizwa jumla ya mabao 5-0 na Mounana ya Gabon nao leo jioni watashuka dimbani kujaribu kuweka rekodi mpya Afrika iwapo wataweza kuwafunga wapinzani wao jumla ya mabaop 6-0 ili waweze kuungana na wenzao wa Yanga waliopenya kwa mbinde juzi usiku baada ya kulala 2-1 ugenini lakini ushindi wao wa nyumbani ukawabeba na kusonga mbele.

Yanga inayotarajiwa kutua nchini leo usiku majira ya saa mbili na nusu ikitokea Gaborone, itaumana na Platnum ya Zimbabwe kati ya Machi 13-15 katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo baada ya Wazimbabwe hao kuing'oa Sofapaka ya Kenya kwa jumla ya mabao 4-2, kutokana na kushinda jana 2-1 kama ilivyokuwa katika mechi ya mkondo wa kwanza nchini Kenya. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.