Habari za Punde

*MABASI YA NGORIKA NA CHATCO YAGONGANA USO KWA USO HUKO MSATA NA KUUA ABIRIA KADHAA

Ajali nyingine ya mabasi ya abiria imetokea leo mchana huko maeneo ya Msata Wilaya ya Chalinze baada ya Basi ya Ngorika na Chatco kugongana uso kwa uso. Katika ajali hiyo imeelezwa kuwa watu kadhaa wamefariki dunia ambapo hadi majira ya saa nane mchana huu tayari jumla ya watu kumi walikuwa wameshasadikiwa kufariki katika ajali hiyo ambao ndiyo walifanikiwa kutolewa.
Raia wakiendelea kuangalia ajali hiyo.
Wasamariawema wakiendelea kukata mabati ya magari hayo ili kuwatoa abiria waliokwama ndani yake.
Ajali hiyo ilisababisha njia hiyo kuwa na msongamano mkubwa baada ya ajali hiyo kufunga barabara.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.