Habari za Punde

*'JULIO AMEYATAKA MWENYEWE', KIPIGO CHA MABAO 8-0 NI HUJUMA AU MGOMO BARIDI WA WACHEZAJI?

BAADA ya timu ya Coastal Union kupokea kichapo cha mabao nane kwa bila katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jana jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wadau wa soka wameibuka na kumlaumu Kocha mkuu wa timu hiyo ya Coastal, Jamhuri Kihwero 'Julio' wakisema kuwa iwapo angeamua kubaki na timu yake ya Mwadui ya Shinyanga, aliyoipandisha Daraja wala yasingemkuta haya yaliyomkutaja jana.

Julio alijiunga na timu hiyo hivi karibuni mara tu baada ya kuipandisha dajara timu yake ya Mwadui na ikaelezwa kuwa ametua kikosini hapo kwa ajili ya kumsaidia aliyekuwa Kocha mkuu wa timu hiyo, Mkenya, James Nandwa, aliyeamua kuondoka kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuwa tayari kufundisha timu moja na Kocha ambaye anauwezo wa kuwa Kocha mkuu. 

Aidha imeelezwa kuwa kwa kipigo cha jana kilichomchanganya Kocha huyo hadi akaanza kuchangua maneno ya kuzungumza na wanahabari, kilichangiwa pia na wachezaji wake ambao wanaonekana kuwa na mgomo baridi wakipinga uwepo wa Julio Kikosini hapo jambo lililomfanya Kocha wao Mkenya kuachia ngazi na kumuachia timu Julio.

Katika mchezo wa jana Julio alimpanga kipa namba mbili wa timu hiyo kufuatia kipa namba moja, Shaban Kado, kutokuwepo Kambini ambaye aliondoka jijini Tanga na kurejea jijini Dar baada ya kutokea kutoelewana na kocha wake huyo.

Habari kutoka kwa wadau wa karibu kabisa wa Klabu hiyo yenye maskani yake jijini Tanga, walisema kuwa kutokana na mgomo huo wa wachezaji inaonekana wanahitaji kocha wao Mkenya James Nandwa, arejeshwe.

''Kiukweli kwa kipigo cha jana kwa timu kama Coastal ni cha kihistoria, haijawai kutokea lazima kuna hujuma au mgomo wa wachezaji wanaonesha kushinikiza kurejeshwa Kocha wao Mkenya, ambaye alionekana kuondoka bila maelewano baada ya kuletwa Kocha Julio''. alisema mdau mmoja wa soka, aliyejitambulisha kwa jina na Majidi Swahib.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.