Wananchi wa jijini Dar es Salaam, wakitembea kwa miguu kuelekea makazini eneo la Jangwani mida hii ya asubuhi, kutokana na mgomo wa Madaladala na Mabasi ya abiria ya mikoani ulioanza leo asubuhi. Katika barabara nyingi za jiji la Dar yanaonekana magari mengi ya watu binafsi huku daladala zikionekana moja moja sana, kama inavyoonekana kwenye foleni hii ya magari eneo la Jangwani yakiwa ni magari madogo ya watu binafsi tu pakiwa hakuna daladala hata moja.
Msafara wa raia ukitembea kwa miguu eneo la Jangwani
Ni mwendo wa masaa kadhaa kuelekea maofisini katika maeneo mbalimbali ya jiji la dar kwa miguu hii leo.
Barabara nyingi za Dar zipo kama hii ya Bibi Titi eneo la Akiba, si kama ilivyozoeleka mida hii ya asubuhi inakuwa imesongamana kwa magari mengi na zaidi zikiwa ni daladala, lakini leo kweupeeee.
Mdogomdogo tutafika maofisini kuwajibika....





No comments:
Post a Comment