Wachezaji wa
vishale (Darts) wa klabu ya Friedz ya Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam, wakiwa
na kikombe chao baada ya kutangazwa kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano
ya mchezo huo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Friendz
walizawadiwa Kikombe na Pesa taslimu Shilingi 100,000/=.
Bingwa wa
mchezaji mmoja mmoja (Singles) wa mchezo wa Vishale (Darts), Erry Boates, kutoka
klabu ya Lugalo akishangilia na kikombe mara baada ya kuibuka bingwa katika
mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
*****************************
Na Mwandishi
Wetu, Dar
KLABU ya Friendz
Wanaume yenye makazi yake Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam wameibuka
mabingwa katika fainali za mashindano ya mchezo wa Vishale(Darts) Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar
es Salaam na hivyo kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi 100,000/=.
Nafasi ya
pili katika mashindano hayo ilichukuliwa na klabu ya Lugalo ambayo ilizawadiwa
pia Kikombe na pesa taslimu shilingi 60,000/=.
Upande wa
Wanawake timu ya Friendz yenye makazi yake palepale Tiptop Manzese ilitwaa
ubingwa wa Taifa na hivyo kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi 60,000/=
wakati nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na klabu ya Kimanga ambao
walizawadiwa kikombe na pesa taslimu Shilingi 40,000/=.
Fainali za
mashinadano ya mwaka huu zilikuwa na mchezo wa mmoja mmoja(Singles) na wawili
wawili (Doubles) kwa Wanawake na Wanaume ambapo upande wa Doubles Wanaume,
Jemes Mlai na Sylivanus Sylivester wote wa Ibukoni klabu waliiibuka mabingwa na
hivyo kuzawadiwa Kikombe na Pesa Taslimu Shilingi 120,000/=, wakati nafasi ya
pili ilichukuliwa na klabu ya Jemes Enea na Nungwa Sadiloa wote wa Polisi Balax
ambao walizawadiwa Kikombe na Pesa taslimu Shilingi 80,000/=.
Upande wa
doubles Wanawake Subira Waziri na Happiness Modaha wote wa Klabu ya Ibukoni
waliibuka mabingwa na kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu shilingi 60,000/=
wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na Fabiola Namajojo na Veronica Sule ambao
walizawadiowa kikombe na pesa taslimu Shilingi 40,000/=
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanaume, Erry Boates kutoka klabu ya Lugalo
alitwaa ubingwa na kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi120,000/= wakati
nafasi ya pili ilichukuliwa na Jemes Enea kutoka Klabu ya Polisi Balax ambaye
alizawadiwa Kikombe na pesa taslimu 60,000/=.
Akizungumza
wakati wa kutoa zawadi aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo, Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Selestine Onditi, aliwashukuru washiriki wote
kwa moyo wa kujitoa kushiriki mashindano ya Kitaifa kutoka katika mikoa mitano
kwa kujitegemea na pili aliwapongeza mabingwa waliofanikiwa na wale ambao
hawakufanikiwa wakajipange kwa mwaka ujao.
Nae
mwenyekiti wa Chama cha Vishale Taifa(TADA), Gesase Waigama aliwashukuru pia
washiriki wote nakuwatakia safari njema za kurudi majumbani kwao pamoja na
maandalizi mema kwa watakaoshiriki mashindano ya mchezo huo ya Afrika Mashariki
yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Mikoa
iliyoshiriki mashindano ya Vishale Taifa mwaka huu ni Mbeya, Morogoro, Dodoma,
Arusha na wenyeji Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment