Habari za Punde

*YANGA BINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA 2015/2016, YAWAVUA UBINGWA AZAMA FC, YAWAADHIBU MAAFANDE WA POLISI MORO 4-1


Wafungaji wa mabao ya leo ya timu ya Yanga, Amis Tambwe (katikati) aliyetupia mabao 3 na Simon Msuva, aliyefunga bao 1 na kufanya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga ya jijini Dar es Salaam na Polisi wa mjini Morogoro, kumalizika kwa matokeo ya 4-1 katika mchezo uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa, wakishangilia mabao yao. katika mbio za kuwania Kiatu cha Dhahabu, sasa upinzani umehamia kwa wakali hao wawili wa timu moja, ambapo sasa Simon Msuva amefikisha jumla ya mabao 17 na Amis Tamwe, mabao 14 huku zikiwa zimesalia mechi mbili, je nani ataibuka kidedea???
*************************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
YANGA leo wamesherehekea matokeo hayo yaliyowatangazia ubingwa na kutwaa Taji la 24 la Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufikisha jumla ya Pointi 55, wakifuatiwa na Azam Fc wenye Poiti 45, huku Simba wanaojaribu kufukuzia nafasi ya pili wakichuana na Azam wakiwa na Pointi 41.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Amis Tambwe, mabao  matatu katika dakika za 40, 53 na 59 na Simon Msuva, aliyemalizia kazi nzuri ya Mrisho Ngassa, huku bao la kufutia machozi la Polisi Moro, likifungwa na Bantu Admin, katika dakika ya 83.

Mara tu baada ya kumalizika kwa mtanange huo, mashabiki wa Yanga walinza kushangilia ubingwa huo huku wengine wakiondoka uwanjani hapo kwa maandamano ya ngoma za mdundiko kuelekea mitaani, ambapo pia shangwe hizo zilianzishwa na Msemaji wa timu hiyo, Jerry Murro, uwanjani hapo baada ya Yanga kupata bao la pili.

Baada ya bao la pili Murro, alianza kuandaa Mafataki uwanjani hapo huku akionekana kuwa bize kuda wote akiandaa taratibu za kushangilia kwa kuwasha mafataki hayo.

Yanga sasa imebakiza michezo miwili kati yao na Azam Fc na Ndanda Fc, ambayo hata ikipoteza michezo hiyo haitawaathiri chochote, kutokana na pointi walizonazo ambazo haziwezi kufikiwa na timy yeyote kati ya hizo mbili zilizo nyuma yake, huku Azam na Simba wakiwa na mchezo mmoja utakaowakutanisha wiki hii. 

Kumbukumbu ya Ubingwa wa Tanzania Bara wa Yanga ni 1968, 1969, 1970, 1971, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011 na 2013, walipovuliwa ubingwa huo na Azam Fc, ambao nao wamerudia kwa aliyewakabidhi ubingwa huo.
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia ushindi wa timu yao uwanjani hapo.
Mfungaji wa bao la Nne, Simon Msuva, akimtoka mchezaji wa Polisi Moro.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.