Habari za Punde

*WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ASISITIZA UWAZI KATIKA MATUMIZI YA TAKWIMU SAHIHI.

 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizindua kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) (Kulia) ni Prof. Ben Kiregyeza, ambaye ndiye mwandishi wa kitabu hicho.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akionyesha kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akimkabidhi moja ya kopi ya kitabu, Prof. Ben Kiregyeza, ambaye ndiye mwandishi wa kitabu hicho, baada ya kukizindua.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akifungua  Kongamano la Kimataifa la Siku 3 la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa awali akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika waliohudhuria Kongamano la Siku 3 la Kimataifa kujadili Matumizi ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.
 Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair akizungumza kabla ya uzinduzi wa  Kongamano  la Kimataifa la masuala ya Takwimu la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa  kutoka Afrika na nje ya Afrika.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.