Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wenzake walioshiriki katika
Mkutano wa dharura wa SADC, mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo kwenye
Hoteli ya Rainbow Jijini Harare, Zimbabwe, jana Aprili 29, 205. Makamu wa Rais
amerejea nchini jana kuendelea na majukumu ya Kitaifa.
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akimkabidhi Katibu
Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax, mfano wa funguo kama ishala ya
makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, wakati
wa Mkutano wa dharura uliofanyika jana Aprili 29, 2015 kwenye Hoteli ya Rainbow
jijini Harare, Zimbabwe.
Kufuatia makabidhiano haya,
Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha
vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani ndani
ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa
mingi katika nchi mbalimbali Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na baadhi ya viongozi wenzake wakitoka
kwenye ukumbi wa mkutano baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa dharura wa SADC
jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya Zimbabwe, huku akipunga mkono kuaga wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Zimbabwe jana Aprili 29, 2015 kurejea nchini. Kushoto kwake ni mkewe mama Zakhia Bilal.
Burudani ya ngoma za asili uwanjani hapo....
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Rajab Adad, wakati
akiondoka kurejea nchini baada ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC, jijini
Harare, Zimbabwe jana.
Kwaherini......

Back to home.....Tanzania







No comments:
Post a Comment