Habari za Punde

*PICHA ZA MTANANGE WA TAREHE COASTAL MWEZI TAMBWE JANA TAIFA

 Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe (kulia) akipokea mpira kutoka kwa  mwamuzi wa mchezo wa Ligi Kuu bara kati ya Yanga na Coastal, uliochezwa jana jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka na mabao manne katika mchezo huo kati ya mabao 8 yaliyofungwa na wachezaji wa Yanga, Simon Msuva, Juma Abdul, Salum Telela na Kpah Sherman.
 Mashabiki wa Yanga wakimjaza mihela mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe baada ya mchezo huo kumalizika jana na kuonyesha kiwango kizuri baada ya kupachika mabao manne kati ya nane.
 Amis Tambwe akionyesha mpira wake aliokabidhiwa jana baada ya mchezo huo.
 Wachezaji wa Yanga, wakishangilia moja kati ya mabao nane waliyofunga katika mchezo huo. Kulia ni Kocha wa Coastal Union Jamhuri Kihweru 'Julio' akishika kiuno bila kujua la kufanya kwa kichapo hicho.
 Haruna Niyonzima (kushoto) na Amis Tambwe, wakishangilia moja kati ya mabao yaliyofungwa na Tambwe.
 Amis Tambwe (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Coastal Union.
 Wachezaji wa Yanga, wakimdhibiti mchezaji wa Coastal, wakati wa mchezo huo.
Beki wa Yanga, Juma Abdul (kushoto) akiambaa na mpira kujaribu kumpita mchezaji wa Coastal.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.