Wachezaji wa Simba wakimpongeza mwenzao, Ramadhan Singano 'Messi' (anayesujudu) baada ya kufunga bao katika dakik ya Nne katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania, Bara uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, huku mabao mengine yakifungwa na Jonas Mkude katika dakika ya 15 na Said Ndemla, katika dakika 21 yote kipindi cha kwanza.
Pamoja na Simba kuibuka na ushindi huo wa mabao 3-0, lakini bado wanaendelea kuwa nyuma ya Azam Fc katika mbio za kuwania nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara, wakiwa na jumla ya Pointi 41 wanika wamecheza mechi 24, huku Azam Fc wakiwa na Pointi 45, wakiwa wamecheza mechi 23 sawa na Yanga wenye Pointi 52.
Azam Fc, wao wamefikisha Pointi hizo baada ya leo kuwachabanga bila huruma, wapiga debe wa Shinyanga, Stand United kwa jumla ya mabao 4-0, yaliyofungwa na Gaudence Mwaikimba mawili, Farid Maliki moja na Brian Majwega moja.
Mchezo mwingine ulikuwa ni kule katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kati ya Wagonga Nyundo, Mbeya City na Wakata Miwa Kagera Sugar, ambapo katika mchezo huo Mbeya City waliibuka na ushindi wa mabao 2-0
Emmanuel Okwi (kulia) akichuana na mabeki wa Ndanda Fc, wakati wa mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa.
Heka heka langoni mwa Ndanda Fc.
Jonas Mkude, akishangilia bao lake alilofunga katika dakika ya 15, huku akipongzwa na Emmanuel Okwi na Said Ndemla.
Awadh (kulia) akimtoka beki wa Ndanda Fc.
Ramadhan Singano Messi, akimiliki mpira mbele ya mabeki wa Ndanda fc.
Emmanuel Okwi, akiwatoka mabeki wa Ndanda Fc.
Wachezaji wa simba wakishangilia mabao yao.







No comments:
Post a Comment