Wanajumuiya wafanyabiashara kutoka
China waishio Tanzania wakimsikiliza Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa
Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja wakati wa
Semina iliyofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa JITENG Consultant
Company Bw. Andrew Huwang akiongea jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China
waishio Tanzania kuhusu ushiriki wao katika masuala ya ukusanyaji kodi na
kuendelea kuongeza ushirikiano kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na
sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa
Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa
Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw.Yeremiah Mbaghi.
Afisa
Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Bw. Hamisi Lupenja akiwaeleza wafanyabiashara kutoka China waishio
Tanzania kuhusu umuhimu wa kushiriki katika matumizi ya Mashine za Risiti za
Kielektroniki (EFD) katika manunuzi na uuzaji wa Bidhaa mbalimbali ili kuiwezesha
serikali kupata mapato stahiki bila udanganyifu wakati wa Semina iliyoandaliwa
na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini
leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Bi. Rose Mahendeka akiongea na jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China waishio
Tanzania kuhusu faida za Mfumo mpya wa Uondoshaji Mizigo (TANCIS) unaosaidia
kuongeza ufanisi katika uondoshaji wa Mizigo ya wateja na kuondoa malamiko ya
ucheleweshwaji wa huduma hiyo pia kuondoa tatizo la upotevu na mizigo pindi
inapoingizwa nchini, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina
waishio Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha
kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment