Kikosi cha Mbeya City. Picha na Maktaba ya Mafoto
***********************************************
Mbio za timu ya Simba Sc za kuwania nafasi ya pili katika
ligi kuu ya Tanzania Bara ziliingia dosari baada ya kufungwa mabao 2-0 na timu
ya Mbeya City.
Wakati Simba Sc ikipoteza kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, wenzao wa
Azam FC walichomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Chamaz Complex na kufufua
matumaini yake ya kuiwakilisha nchi katika moja ya mashindano ya CAF.
Azam Kwa sasa ina pointi 42, nne nyuma ya Yanga inayoongoza
ligi hiyo ikiwa na pointi 46.
Hata hivyo Azam FC imeizidi Yanga mechi moja.
Mbeya City ilicheza vizuri katika mchezo huo na mabao yake yalifungwa na Paul
Nonga na Peter Malyanzi.
Na kwa upande wa
Azam Fc, mabao yake yalifungwa na Frank Domayo na Gaudence Mwaikimba, huku bao la mwaikimba likizua utata mkubwa.

No comments:
Post a Comment