Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, akimtoka beki wa Etoile Du Sahel, wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imelazimishwa sare na waarabu hao wa Tunisia, ambapo Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 1, lililofungwa na Naidir Haroub 'Canavaro' kwa mkwaju wa penati baada ya Simon Msuva kuchezewa rafu katika eneo la hatari. Bao la Etoile Du Sahel, lilifungwa na ....katika dakika ya
****************************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar es Salaam
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la
Shirikisho, Yanga wanakabiliwa na
kibarua kigumu kusonga mbele hatua ya mwisho ya mtoano baada ya kutoka sare ya
bao 1-1 dhidi ya timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia.
anga ya Jijini Dar es Salaam, itakuwa na kibarua kigumu katika mchezo wake wa marudiano na timu ya Etoile Du Sahel unaotarajiwa kuchezwa baada ya wiki mbili huko Tunisi, baada ya leo kulazimishwa sare na waarabu hao ya bao 1-1 katika mchezo uliokuwa mgumu kwa timu zote huku waarabu wakionekana kushambulia kwa kijihami zaidi dakika zote.
Yanga inatakiwa kushinda au kutoka sare ya mabao kuanzia
mawili katika mchezo wa marudiano uliopangwa kufanyika mjini Tunis wiki mbili
zijazo. Endapo timu hiyo itatoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu hiyo, italazimika
kupigiana penati ili kumtafuta mshindi.
Tofauti na michezo mengine iliyopita dhidi ya BDF XI ya
Botswana na FC Platinum ya Zimbabwe, Yanga ilicheza vizuri katika mechi zote
mbili, lakini katika mchezo dhid ya
Etoile, vijana hao wa Jangwani walishindwa kufurukuta richa ya kuongoza kwa bao
1-0 hadi mapumziko.
Yanga ilianza mchezo kwa kasi na kupata bao kwa njia ya
penati katika dakika ya pili baada ya kipa wa Etoile, Mathlouthi Aymen
kumwangusha Simon Msuva ambaye tayari alikuwa amempiga chenga na kujianda
kufunga.
Nahodha wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
na ile ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) alifunga penati hiyo. Etoile ilisawazisha
katika dakika ya 47 kupitia kwa Ben Amor
Med Amine ambaye alipiga shuti nje ya eneo la hatari na kumpita kipa wa Yanga
Ali Mustafa.
Beki wa Etoile, akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe.
Amis Tambwe, akijilaumu baada ya kukosa bao.....
Mashabiki wa Etoile, wakishangilia bao la timu yao.....
Amis Tambwe, akiwania mpira na beki wa Etoile. KATIKA MECHI ZA LIGI KUU BARA, MBEYA CITY 2-SIMBA 0
AZAM FC 2- KAGERA SUGAR 1
KWA PICHA ZAIDI ZA MTANANGE HUU, KAA NASI BAADAYE.






No comments:
Post a Comment