Mkurugenzi Habari na Mahusiano wa JKT Kapteni Javan Bwai akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya SUMAJKT kupitia kampuni
ya ujenzi ya NSCD katika kipindi cha miaka 10 ya awamu ya nne ambapo alisema
miradi 18 ya ujenzi imekamilika na miradi 9 inaendelea kujengwa . Kulia ni
Kaimu Msemaji Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Meja Josephat Musira
na kushoto ni Mkurugenzi wa ufundi SUMAJKT Mhandisi Fredrick Kaaya.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakiwasikiliza viongozi wa JKT walipotembelea jengo
la kitega uchumi cha Kanisa la KKKT
‘’Msasani Tower’’ lililopo Msasani jijini Dar es Salaam ambalo
limejengwa na kampuni ya ujenzi ya JKT (NSCD).
Koplo Mhandisi Lazaro Masanja kutoka Wizara
ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akitoa rai kwa wananchi na Taasisi kutumia Shirika la Uzalishaji Mali
la JKT (SUMAJKT) kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa gharama nafuu. Nyuma
ni jengo la kitega uchumi cha Kanisa la
KKKT ‘’Msasani Tower’’ lililopo Msasani
jijini Dar es Salaam ambalo limejengwa na kampuni ya ujenzi ya JKT (NSCD). Picha na Georgina Misama -MAELEZO
No comments:
Post a Comment