Mwalimu
Veronika Mtes wa shule ya msingi Kibirizi aliyepata mshtuko baada ya tukio
la radi akiwa katika hospitali ya Mawenzi mkoa wa Kigoma akipatiwa matibabu.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Kigoma,Maweni akiongeza
na Waandishi wa habari juu ya tukio la radi lililotokea jana na kuuwa watu 8,
mkoani Kigoma.
************************************************
Na Editha
Karlo,Kigoma
WATU
wanane wanafunzi sita na mwalimu wa shule ya msingi kibirizi na mkazi wa eneo
la Bangwe mjini hapa wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi huku wanafunzi
wengine 15 wakijeruhiwa na radi hiyo mchana wa jana.
Mganga
mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa kigoma (maweni) Dkt Fadhili Kabaya,
alisema kuwa watu hao walifikwa na umauti kufuatia mvua kubwa
zilizonyesha zikiambana na radi zilizoanza majira ya saa sita mchana.
Dkt
Fadhili aliwataja waliofariki katika tukio hilo kuwa ni pamoja na mwalimu wa
shule ya msingi Kibirizi, Elinaza Mbwambo (25) Forcus Ntahaba (45) mkazi wa
eneo la Bangwe mjini hapa.
Aliwataja
wanafunzi waliofariki ambao wote ni wa darasa la kwanza kuwa ni Yusuph Ntahoma
(8) Hassan Ally (9) Fatuma Sley (7) Zamda Seif (8) Shukranmi Yohana (7) na
Warupe Kapupa (10).
Aidha,
alisema walipokea majeruhi 15 lakini kati yao 10, waliruhusiwa baada ya
kupatiwa matibabu baada ya hali zao kuwa nzuri na watano wamelazwa wanaendelea
na matibabu katika hospital ya Mkoa wa Kigoma.
Akisimulia
tukio hilo mwalimu aliyekuwa anafundisha darasani Mwalimu Merina Sililo,
alisema kuwa akiwa darasani akiendelea kufundisha ghafla aliona wingu
zito jeusi limetanda hali iliyompelekea kushindwa kuendelea kufundisha kutokana
na giza nene.
''Manyunyu
yalianza kidogo kidogo ikaja mvua kubwa na radi pamoja na miungurumo mikali
iliyopelekea wanafunzi kuanguka hovyo darasani na kuzimia, na mara
niliona moto umetanda katika chumba kizima cha darasa na mimi nilianguka chini
na kupoteza fahamu''alisema mwalimu huyo
Alisema
alipozinduka alijikuta katika hospital ya Mkoa akipatiwa matibabu baada ya
kufikishwa kwa msaada wa waalimu wenzake.
''Kwakweli
ni mungu tu mwenyewe ndo ameninusuru kwani nilirushwa mara tatu na radi na
watoto wote darasani walikuwa wananiangukia mimi wengine walikuwa wanakimbia
hovyo nje''alisema Mwalimu huyo. (Muro)
No comments:
Post a Comment