Habari za Punde

*WAZIRI CHAWENE, AFUNGUA MAONESHO YA KIMATAIFA YA VITO NA MADINI JIJINI ARUSHA

 Waziri wa Nishani na Madini Mhe. Simba Chawene, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Maonyesho ya Nne ya Kimataifa ya Vito yaliyoanza jijini Arusha jana. Kulia ni Kamishna wa Madin, Paulo masanja. 
  ************************************
Na Miraji Msala, Arusha
Maonesho ya 4 ya Kimataifa ya Vito na Madini yanayo husisha nchi za Afrika Mashaliki na Kati yalifunguliwa rasmi na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Simba Chawene, jijini Arusha na 

Maonesho hayo yalihudhuliwa na Viongozi mbali mbali wa Wizala hiyo pamoja na wachimbaji madini, watengenezaji na wanunuzi ambao ni wateja wakubwa katika sekta hiyo.

Kusudi kubwa la kuandaa maonyesho hayo ni kuwakutanisha wadau mbali mbali ndani na nje ya nchi na kuonyesha kazi zao sambamba na hilo ni fulsa nzuri kwao kwa ajili ya kutanua masoko.

Baadhi ya wageni waliohudhuria maeonesho hayo ni pamoja na ujumbe kutoka nchi za Ujerumani, China, Marekani pamoja na nchi mbalimbali za Afrika.

Akizungumza na wanahabari Waziri Chawene, baada ya ufunguz huo alisema kuwa maonesho hayo ya vito ya kimataifa kwa safari hii yamekua na mvuto mkubwa zaidi ya yale yaliyopita kutokana na mwitikio wa wageni waalikwa kutoka nchi mbalimbali.

Aidha aliwapongeza wachimbaji na hasa watengenezaji wa vito wa hapa nchini kwa viwango vikubwa vya kimataifa wanavyo vionyesha katika maonesho hayo.

''Nimeguswa sana na maonesha haya, kuna watanzania wengi wanaishia kupoteza matumaini na kuzeekea kwenye migodi wakijiita wachimbaji wadogo  sasa basi watu hawa wanaweza kujifunza fani ya ukataji na utengenezaji wa vito ambayo inaweza kuwapatia kipato kikubwa tofauti na kuvunjika moyo wakiwa huko migodini,

Selikali inamikakati na tayari imesha anza kujenga vyuo vya kutoa mafunzo katika eneo hilo sanjali na hilo alitoa ufafanuzi wa jinsi selikali ilivyo jipanga kukabiliana na watoroshaji wa vito kupitia kitengo chake cha T.M.A.A  ambapo kupitia kitengo hicho tumefanikiwa sana''. alisema Chawene
 Kamishina wa madini Eng. Paul Masanja akitoa utangulizi na kumkaribisha mgeni rasmi Mhe. Simba Chawene.
 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Simba Chawene, akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo na kuwakaribisha wageni.
 Baadhi ya wadau wa Madini waliohudhuria maonesho hayo wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi huo jana kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru.
 Waziri Chawene, akimsikiliza mmoja wa wachimbaji madini wakati akitoa maelezo huhusu shughuli za uchimbaji wakati Waziri huyo alipotembelea katika mabanda ya maonesho.
 Waziri Chawene (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wachimbaji kutoka Rwanda.
  Wazili Chawene, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizaya yake. 
Waziri Chawene, akizungumz na waandishi wa habari baada ya ufunguzi huo. Picha Zote na Miraji Msala, Arusha

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.