Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joeli Bendela, akikata utepe kufungua rasmi Maadhimisho 18 ya wiki ya
Maziwa Kitaifa Mkoani Manyala, Kulia Kwake ni Mwenyekeiti wa Bodi ya Maziwa, Dk. Aichi Kitalyi.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendela, akitembelea baadhi ya Washiliki
Katika Maonyesho hayo ya 18 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa Mkoani Manyala, hapa akipata maelekezo kutoka kwa mfugaji, George mkazi wa Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendela, akitembelea baadhi ya Washiliki Katika mabanda ya maonyesho hayo ya 18 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa Mkoani Manyala, hapa ni wakati akipata Maelekezo kutoka kwa Stanly Wafula, Mmoja kati ya Washiliki wa maonesho hayo wa Bidhaa za Maziwa.
Mwenyekiti Bodi ya Maziwa Dr, Aichi Kitalyi, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi na wageni waalikwa katiaka maadhimisho hayo ya 18 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa Mkoani Manyara.
Mwakilishi Kutoka Wizara ya Maendereo ya Mifugo na Uvuvi, ambaye ni Afisa Mifugo Mkuu wa MLFD, Abdallah Temba, akiongea na washiliki katika Maadhimisho ya wiki ya Maziwa Kitaifa Mkoani Manyara
M kuu wa Wilaya ya Babati, Francins Mitti, akimkalibisha Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo.
Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh, Joeli Bendela, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya 18 ya wiki ya Maziwa Kitaifa Mkoani Manyara, ambapo alielezea lengo la maonesho hayo kuwa ni kuwakutanisha wadau mbalimbali katika sekta hiyo ya Ufugaji na Usindikaji wa Maziwa ili kupata changamoto ya kuona wengine wanavyo fanya na kubadilishina uzoefu ambao utawawezesha kufanikiwa katika ufugaji na usindikaji wa kisasa.
Kikundi Cha Ngoma cha Msanja kutoka Babati Mjini Kikitumbuiza katika Maadhimisho hayo.
Glagness H. Kaseka akizungumza na waandishi juu ya ushiliki wake kama TBS, ili kutoa elim juu ya usindikaji wenye viwamgo vitakavyo kubalika kuuza bizaa zao ndani na nje ya nchi. Picha na Miraji Msala
No comments:
Post a Comment