Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo leo bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Said Mtanda akiwasilisha mapendekezo ya kamati yake kuhusu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa bajeti ya wizara hiyo leo mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kutoka kushoto) wakifuatilia kwa makini bajeti ya Wizara hiyo leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma. PICHA ZOTE NA FATMA SALUM - MAELEZO
*****************************************************
Abraham Nyantori MAELEZO, Bungeni, Dodoma
Serikali
imeshauriwa kutenga fedha za kutosha ili kuiwezesha Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Ushauri
huo umetolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakati wa
kuwasilisha mapendekezo yake leo bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa kamati Mhe. Said Mtanda amesema Wizara hiyo ina jukumu la kuratibu na kusimamia maendeleo ya vijana, utamaduni,
michezo na habari hivyo ikipewa fungu la kutosha itaweza kuleta mabadiliko
chanya kwenye sekta hizo.
Akiwasilisha
Bajeti ya Wizara yake bungeni leo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara ameliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya wizara hiyo ya shilingi bilioni 29.4 ambapo shilingi bilioni 5 ni kwa ajili ya
maendeleo na shilingi bilioni 24.4 ni matumizi ya kawaida.
Aidha Waziri Mukangara ameeleza jitihada
mbalimbali zinazofanywa na wizara yake zikiwemo kuratibu na kuwajengea vijana
uwezo wa kubuni mawazo bora ya kujiajiri, kuhamasisha halmashauri kutenga
asilimia 5 ya bajeti yao kuboresha mifuko ya vijana na kuhamasisha uanzishaji
wa SACCOS.
Katika
mwaka wa fedha uliopita wa 2014/2015, Waziri Mukangara amesema wizara yake
ilitoa mafunzo kwa vijana 1550 katika kujenga dhana ya kujiajiri, na jumla ya shilingi bilioni 2 zilikopeshwa kwa vikundi
mbalimbali vya vijana kote nchini.
Kwa
upande mwingine Dkt Mukangara amesema wizara yake imekamilisha miradi kadhaa ukiwemo
mradi wa Mawasiliano na kukamilisha lengo la milenia la kubadili matumizi ya analojia kwenda
dijitali, mradi huo ulikamilika mwezi Aprili mwaka huu. Miradi mingine katika
mwaka wa fedha uliopita ilikuwa ni ya utafiti ukiwemo wa msamiati wa lugha za
jamii, utafiti wa majina fiche 1800 ya lugha za asili.
Wizara
katika mwaka huu wa fedha imeahidi kuongeza ufanisi ikiwemo kuongeza ajira kwa
vijana, kulinda mazingira, kutoa habari,
kulinda mila na desturi kudumisha amani na mshikamano wa katika jamii ya
watanzania.
Leo
ni siku ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Wizara ya Maliasili
na Utalii ambazo zimewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara zao na
hatimaye kuruhusu Bunge kuendelea kuzijadili bajeti hizo.
Mitambo ya kukodi TBC na uchaakavu wa majengo, madeni 3.2 /1.3 serikali.
Katika
kipindi cha 2014/15 wizara ipanga kukusanya sh. 1,149,008,000 kutoka vyanzo
mbalimbali zilizokusanywa ni sh. 811,616,116 sawa 71%
Wizara
ilitengewa (2014/2015) 19,806,611,000 zilipokelewa sh.
14,446,963,490 sawa na 73% ya bajeti ya matumizi ya kawaida. Fedha za maendeleo
wizara 2014/15 ilitengewa 16,850,000,000 ilipokea hadi april
2015 >7,000,000,000 sawa 42% upanuzi wa usikivu wa shirika la
utangazaji la Tanzania TBC
Moja
ya changamoto ni kuongezeka kwa mifumo na njia za mawasiliano kwa umma kama
mitandao ya jamii kwenye intanet kunakoadhiri maudhui ya taarifa zinazotolewa
Wizara
kukabiliana na changamoto hizo imetoa elimu na kutembelea vituo kwa kushirikia
na kamati ya maudhui (TCRA)
No comments:
Post a Comment