Rais Mstaafu wa awamu wa pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Baraza la Usuluhishi la Jamhuri ya Iran, Ayatollah Rafsanjani jijini Tehran,jana.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaji Ali Hassan Mwinyi, akikata Keki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Siku ya Afrika. W tatu (kulia) ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Dkt. Zariff, pamoja na baadhi ya Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo.
*************************************************
Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Alhaj Ali Hassani Mwinyi, amefanya ziara ya siku tatu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ziara hiyo ya Rais Mstaafu inafuatia mwaliko wa Serikali ya Jamhuri hiyo ya Kiislamu ya Iran
uliomuomba kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuadhimisha miaka 52 ya Afrika.
Siku ya Afrika huadhimishwa kila tarehe 25 Mei
na mataifa ya Afrika pamoja na Mabalozi na Wawakilishi wamataifa hayo duniani kote,
ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kuasisiwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) tarehe 25
Mei 1963.
Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
imejiwekea utaratibu wa kuungana na Waafrika pamoja na wadau wengine wanaounga mkono hatua za ukombozi na kupinga ubeberu katika maadhimisho ya siku hii muhimu.
Katika sherehe hizo,
Rais Mstaafu Mwinyi alihutubia hadhira iliyoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
Dkt Muhammad Javad Zariff na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wawakilishi waliopo Iran,
Viongozi na Maafisa waandamizi wa Serikali ya Iran,
na wadau wengine muhimu ikiwemo wanataaluma, wawakilishi wa sekta binafsi na wanahabari.
Aidha,
Rais Mstaafu Mwinyi alipata nafasi ya kukutana na Mkuu wa Kamisheni ya Usuluhishi ya Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran ambaye pia ni Rais Mstaafu wa taifa hilo Ayatollah Hashemi Rafsanjani.
Ayatollah Rafsanjani alikuwa Rais wa Iran wakati Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais wa
Tanzania
na wawili hao waliimarisha uhusiano wa kidiplomasia wa mataifa haya mawili ambapo kila mmoja alizuru nchi ya mwenziwe.
Rais Mstaafu Mwinyi aliupokea mwaliko wa taifa hilo kwalengo la
kuzidi kuimarisha uhusiano wa kidugu baina ya Tanzania na Iran. Katika ziara hiyo,
Rais Mstaafu Mwinyi aliongozana na Mkewe, Mama Khadija Mwinyi.


No comments:
Post a Comment