Habari za Punde

*AIRTEL YAWAZAWADIA WATEJA WAKE MARA TANO ZAIDI MUDA WA MAONGEZI

Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano, akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofa ya "Kamata Tano Zaidi" inayowawezesha wateja wa Airtel kupatanmara tano ya muda wa maongezi.
*******************************************
Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel leo imezindua ofa kabambe kwa wateja wake wa Airtel Money ijulikanayo kwa jina la "Kamata tano Zaidi" itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata muda wa maongezi mara 5 zaidi pindi watakaponunua muda wa maongezi au yatosha zaidi kupitia Airtel Money.
Akizungumza katika uzinduzi, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Airtel , Arindam Chakrabarty alisema, kuanzishwa kwa bonus ya mara 5 zaidi kwa kununua muda wa maongezi kupitia Airtel Money ni katika juhudi za Airtel kuendeleza dhamira na azma yao ya kuwajali na kuwazawadia
wateja .
"Lengo letu ni kutoa huduma nafuu, zenye ubora, tija na zinazokidhi mahitaji ya mawasiliano kwa wateja wetu nchini kote. Nina imani "Kamata Tano Zaidi" italeta uhuru wa kuwawezesha wateja wetu kuwasiliana na familia zao, marafiki na hasa kuongeza ufanisi katika biashara zao popote pale walipo . "
"Chakrabarty aliongeza kwa kusema, " tunawaahidi wateja wetu kupitia huduma ya Airtel Money tutaendelea kuwapa huduma za kisasa na kuwazawadia mara 5 ya matumizi yao kama bonus ya muda wa maongezi itakayowawezesha kupiga simu kwenda namba yoyote ya Airtel kwa siku hiyo".

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa AirtelTanzania, Beatrice Singano, alisema, "Bonus ya mara 5 zaidi itapatikana kwenye aina zote za manunuzi ya muda wa maongezi yatakayonunuliwa kwenye mfumo wa Airtel Money kwa kupiga *150*60# na kuchagua namba 2. Muda wa maongezi utakaonunuliwa utajumlisha muda wa maongezi wa kawaida pamoja na vifurushi vyote vya Yatosha au Yatosha Noma. Bonus ya mara 5 zaidi ya "Kamata Tano Zaidi" inayopatikana kwa kununua kupitia Airtel Money itadumu kwa muda wa masaa 24 toka muda uliponunuliwa, ili kuwatimizia wateja wetu mahitaji yao ya mawasiliano

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.