Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa
Shinyanga, Hamis Mgeja akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani
) kuhusu kung'atuka katika chama hicho na kujiunga na Chadema wakati wa mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, jana. Kulia ni John Guninita.
Aliyekuwa, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa
Shinyanga, Hamis Mgeja akionesha alama ya vidole viwili kuashiria kuwa yeye ni chadema kwa sasa, baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Maelezo jijini Dar es Salaam, jana.
************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja ametangaza rasmi kuachia ngazi na wadhifa wake huo na kutimkia kwa wazee wa vidole viwili CHADEMA.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, jana, Mgeja alisema kuwa
ametafakari kwa makini kabla ya kutangaza uamuzi wake huo na kuna kila sababu za kujiunga na wapinzani wake Chadema.
Mgeja alisema kuwa ameamua kuachia ngazi na kwenda kutafuta
mabadiliko katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kukitumikia Chama hicho cha Mapinduzi tangu enzi za Mwalimi Nyerere na kuongeza kuwa hivi sasa imefika wakati wa kuondoka.
Aidha alisema kuwa CCM ya sasa imekuwa na vitu
ambavyo vinafanywa na watu na baadaye kukigharimu chama kutokana na kuacha msingi
wa kukubali maoni ya wanachama.
Naye aliyekuwa
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita naye alitangaza kuachana na chama hicho na kujiunga na Chadema ili kuongeza nguvu katika umoja wa Ukawa.
Guninita alisema kuwa sasa umefika wakati wa
kuondoka kutokana na uongozi wa Chama kuacha kusikiliza maoni ya wanachama wake na badala yake
kuendeleza chuki ndani ya Chama.
No comments:
Post a Comment