Kijana Khatib Salum (27) akimsuka mteja wake aliyejitambulishwa kwa jina la Sophia Shaaban, mkazi wa Kijiji cha Ngiloli, Gairo. KIjana huyo amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda mrefu sasa ambapo wateja wake wamekuwa wakimpigia simu 0716560572, ili kupata huduma yake kwa Sh. 500,000/-kwa kila kichwa. Salum amekuwa akisuka watu watatu hadi wanne kwa siku kutegemea na msuko wa mteja, huku wateja wakimpigia simu ili awafuate na kuwapa huduma yake mahala walipo.
Hapa Kijana huyu alikuwa akifanya kazi yake hii pembezoni mwa barabara ya Dodoma-Morogoro katika kituo maarufu kwa kuuza Nayanya, Maharage, Vitunguu na vinginevya cha Ngiloli, huku pembeni jamaa akilinda mzigo wake upendeze. Hata hivyo kijana huyu aliomba msaada wa kupata kibarua katika Saluni za jijini Dar es Salaam ili aweze kuongeza ujuzi wake na kufaidika na kazi ya mikono yake.
''Natamani kufika jijini Dar kama nikipata mfadhili ili niweze kufanya kazi katika Saluni kubwakubwa na mimi niweze kufaidika na kazi za mikoni yangu, kwani nimesikia Dar mtu mmoja husukwa kwa kiasi kikubwa cha fedha lakini mimi huku kijijini ni Sh. 500,000 tu,
Nawaomba Wenye Saluni kubwa kubwa za jijini Dar wanisaidie niweze kuendeleza kipaji changu, mimi nipo tayari kufanya kazi ili mradi tu nihakikishiwe mshahara na pa kuishi''. alisema Salum
Kazi ya ususi ikiendelea kwa umakini mkubwa....
Ni hadi apendeze.....




No comments:
Post a Comment