Habari za Punde

*MAMA SAMIA SULUHU AUNGURUMA NDANI YA SINGIDA

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Mkalama, Allan Kiula, katika mkutano uliofanyika katika jimbo hilo leo.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, katika mkutano uliofanyika katika jimbo hilo leo. 
 Wananchi waliojawa na furaha wakimkimbilia kumlaki, Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, alipowasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika viwanja vya Kyengege, Iramba mkoani Singida leo.
 Umati wa wananchi ukimsikiliza Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu alipohutubia mkutano wa kampeni katika eneo la Msange, Singida Kaskazini, leo.
 "Baba hakimbii nyumba" Kijana akiwa na bango linalowasema wanaaokimbia  kutoka CCM kwenda upinzani kutokana na kutochaguliwa katika nafasi za uongozi, kijana huyo alipokuwa kwenye mkutano wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, uliofanyika leo Iramba mkoani Singida.
 Mgombea Ubunge jimbo la Iramba Magharibu, Mwigulu Nchemba akiomba kura, wakati wa mkutano wa kampeni za CCM wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, uliofanyika leo katika jimbo hilo.
Mgombea Ubunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba akiselebuka na baadhi ya viongozi na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika eneo la Kyengege, Iramba mkoani Singida, leo. Picha na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.