Habari za Punde

*MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA MITAA YA MJI WA KIGOMA LEO, MWANADADA ATEMBEZA KICHAPO KWA WANANCHI

  Binti aliyejulikana kwa jina la Sinina Maliki,aliyedaiwa kuwa amechanganyikiwa, akiwa ameshikiliwa na wasamalia wema baada ya Binti huyo kutembeza kichapo kwa wananchi na hatimaye kudhibitiwa watu hao waliofanikiwa kumtia nguvuni na kumpeleka nyumbani kwao chini ya ulinzi Mitaa mji wa Kigoma leo.
Ajali ya Gari la Cocacola lenye namba za usajili T282 ALM, likiwa limeanguka. 
Kijana, aliyejitambulisha kwa jina la Eflahim Maksoni, akiwa amepanda Baiskeli huku akipita juu ya Reli maeneo ya Nguruka Mkoani Kigoma, (Hii pia ni fani aisee)
 Baadhi ya Abiria wakiteremka ndani ya Basi katika Kituo kipya cha Mabasi cha Masanga Gungu mkoani Kigoma.
kijana mwendesha baiskeli akiwa amewapakia watoto wawili.
 Wafanya biashara wa chumvi wakiwauzia abiria wa Kigoma
 Mwenyekiti wa Mtaa Sido na Mgombea Udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Murubona akiwa na wafuasi wake juzi  waliomsindikiza Ofisi ya chama Wilaya kata ya Kusenga wilaya ya Kasulu Mkoa Kigoma. Mgombea huyo aliwasilisha malalamiko baada ya kumshinda mwenzake katika kura za maoni ambapo yeye alipata kura 183 na mpinzani wake kupata kura 139 katika kinyanganyiro cha kura za maoni na hatimaye ushindi kupewa mwenzake
 Wakichota maji eneo la Kaliua katika kituo cha mabasi
Wananchi wakikata  tiketi katika kituo kipya cha Stendi ya mabasi ya Mikoani kilichopo Masanga Gungu mkoani kigoma, ambapo kuingia kituoni hapo na kutoka kila mtu hutozwa kiasi cha Sh. 200.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.