Habari za uhakika kutoka ndani ya familia ya mshindi
wa shindano hilo zinasema kuwa vikao vya mara kwa mara hufanyika kupanga
mkakati wa kuvamia ofisi za BASATA kujua hatma ya binti yao Yolanda shayo.
ILIKUAJE:
Wakati wa kutangaza matokeo ya ushindi siku ya
fainali za mashindano hayo usiku wa julai 24,mshindi alikabidhiwa Televisheni
kama zawadi na kiasi cha pesa kilichoadiwa kutolewa na mdhamini mkuu ambae ni
Coca cola.
Cha kustaajabisha muandaji huyo alienda ofisi za
kampuni hiyo na kuchukua kiasi hiko cha fedha ikiwa ni zawadi ya mshindi wa
kwanza lakini mpaka leo mrembo huyo anahaha kupata zawadi yake.
Yolanda aliamua kufunga safari mpaka ofisi za Bonite
Bottles na kuwauliza wahusika kuhusu zawadi yake na alijibiwa kuwa muandaji
huyo alishakabidhiwa fedha hizo siku nyingi.
Mrembo huyo alichukua hatua nyingine ya kumpigia simu
Jackline na kumuulizia kuhusu zawadi yake ya fedha taslimu alioadiwa jukwaani
na wadhamini wakuu,chakushangaza muandaaji huyo alitoa kauli ya kumvunja moyo
kwa maana hatoipata kabisa kwa kisingizio eti hakupata faida.
FAMILIA YA YOLANDA:
Familia ya mrembo huyo imechukizwa na kitendo cha
muandaaji huyo kwa kuingia mitini na zawadi ya binti yao na bila kumkabidhi
mikononi mwa kampuni hiyo ambapo ilitoka ahadi kuwa atakuwa balozi wa kampuni
hiyo kufanya kazi mbalimbali kama balozi wa kinywaji hiko mkoani humo.
Wazazi wa mrembo huyo wamedhamilia kutinga ofisi za
BASATA kufatilia mkataba wa bitni yao kutokana hali ya sintofahamu kuendela
toka binti yao atawazwe kuwa mshindi mnamo julai 24.
Pia wanafamilia wametoa shutuma nzito kwa shindano
hilo wakihoji ni kwanini msanii wa bongo flava anapewa milioni 25
kutumbuiza wakati binti yao ambae ndiye mshindi anambulia zawadi ya televisheni
pekee.
WASHIRIKI WENGINE:
Hali ni tata pia kwa washiriki
wa walioingia tano bora hasa namba nne ambae alizawadiwa laki nne na mapazia
kutoka kampuni ya Mapazia house lakini chakushangaza muandaji huyo aliingia
mitini na fedha hizo na kumuacha mrembo akirudi nyumbani na mapazia tu.
Mrembo huyo Willice Donard amelalamikia kitendo cha
muandaji huyo kumjibu majibu ya dharau pale alipompigia simu kuulizia zawadi
yake.
Habari zinasema kuwa mrembo alieshika namba tano,Femy
Lema alipokonywa nusu ya kiasi cha fedha alichokabidhiwa jukwaani ikiwa ni
zawadi ya kuingia tano bora.
KAMATI YA MAANDALIZI:
Hali si shwali kwa upande wa kamati,habari za uhakika
toka kwa watu walioshiriki kumpa sapoti muandaaji huyo zikizadai
kuwa amewaingiza chaka na kuwazulumu haki yao ya malipo,mpaka sasa hawajui
fedha zao watazipataje.
KAULI ZA MUANDAAJI:
Kauli za muandaji zilizojaa dharau na kejeli kwa watu
wanaodai haki zao ndizo zilizowapandisha hasira na kufanya baadhi ya watu
kutoboa ukweli huu kwani amekuwa akiwaambia anaenidai aende mahakamani huko
ndiko haki ya mtu hupatikana kwa kisingizio eti amesomea sheria.
KUMBUKUMBU ZAKE:
Kumbukumbu za muandaaji huyu zinaonesha ni mtu ambae
anapenda mambo ya ujanja-ujanja na kujipatia faida kubwa kupitia majina ya watu
kama alivyotaka kumtumia Zari Hassan kuvuta watu wengi kuingia katika tamasha
lake na angali hakuwa na mkataba wowote na Zari.
Kitendo hiko kilimfanya Diamond Platnumz kutaka
kususia na kuandika maneno makali katika ukurasa wake wa instagram,kitu
kilichompelekea kutozwa faini na uongozi wa Zari.
BASATA:
Wito umetolewa kwa balaza la sanaa kuwa makini kwa
kutoa vibali kwa waandaji wasio na uhakika na shughuli wanazofanya kama
ilivyotokea kwenye hili shindano la Miss Kilimanjaro Ambassador 2015.
Tunaamini dhamira ya shindano hili ni nzuri na lina
manufaa kwa jamii kuhusiana na utalii,utamaduni na kazi za kijamii,shindano
hili lina faida ila tatizo liko kwa muandaaji mwenyewe kana kwamba hana malengo
na shindano hilo.
Lawama za pekee ziende kwa Basata kwani shindano hili
lilipelekwa kienyeji bila usimamizi wowote kama ilivyo kwa mashindano mengine
makubwa,isitoshe kanuni na taratibu hazikufuatwa mwanzo mwisho ndiyo maana leo
tunapata malalamiko ya mshindi Yolanda shayo kuingizwa mitini zawadi na mkataba
wake.

No comments:
Post a Comment