Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Peacock leo jijini Dar es salaam wakati akitangaza kujuuzulu nyazifa zake zote katika chama hicho na kubaki mwanachama wa kawaida kutokana kile alichokiita dhamira inamsuta.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akionyesha rasimu ya katiba iliyoandaliwa na tume ya katiba mpya iliyokuwa ikipendekezwa iliyoandaliwa na Jaji Joseph Warioba ambayo anadai imefinyangwa. Lipumba alionyesha Rasimu hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,leo.********************************************
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu kama mwenyekiti wa chama hicho akisema dhamira inamsuta.
Profesa Ibrahim Lipumba, amezungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo, ambapo alisema kuwa amejitahidi kujenga chama hicho hasa Tanzania bara, amejenga umoja wa Wazanzibari hivyo anajiuzulu kulinda heshima yake.
Amesema ameikabidhi Ofisi ya Katibu Mkuu, barua yake ya kung’atuka nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, lakini ataendelea kuwa mwanachama wa CUF na kadi yake imelipiwa mpaka mwaka 2020.
Ameeleza sababu za kujiuzulu ni Umoja wa huo wa UKAWA kushindwa kuenzi Tunu za Taifa katika umoja wao kwa kuwakaribisha watu waliopitisha rasimu iliyochakachuliwa kwenye Bunge Maalumu la katiba.
Profesa Lipumba amekiri kushiriki katika vikao mbalimbali vya Ukawa mpaka hapa walipofikia . lakini akasema, nafsi yake inamsuta kuwa katika maamuzi ya kushindwa kuenzi na kuzingatia Tunu za Taifa na utu, uadilifu, uzalendo, uwajibikaji,, umoja, na uwazi.
Aidha amesema ametafakari kwa makini sana katika kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho lakini dhamira yake inamsuta.
Amesema kuwa mwaka 2014 hakutaka kugombea nafasi hiyo kutokana na mchakato wa katiba mpya akaamua kugombea kwa lengo ya kuwapa watanzania katiba itakayoindoa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lipumba amesema katika mchakato wa bunge maalumu wakaunda umoja wa katiba (UKAWA0 wenye lengo wa kusimamia katiba iliyopendekezwa lakini sasa waliopitisha ndio wanataka kuisimamia katiba hiyo ambayo haingii akilini.
Amesema alikuwa akishiriki vikao vya UKAWA lakini Aprili 1 mwaka huu alisema atang'atuka katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wanannchi (CUF).
Amesema amepita katika misukosuko mingi katika kukijenga chama hadi kufikia kiasi hata kabambikiziwa kesi ya kufanya maandamano bila kibali.
Lipumba amesema kazi yake atakuwa mwanachama wa kawaida, kufanya utafiti wa maendeleo endelevu pamoja na kufanya ushauri wa masuala mbalimbali katika chama hicho.
No comments:
Post a Comment