Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea hati ya utambulisho
ya Balozi wa Denmark nchini Tamzania Einar Hebogard Jensen (kulia) leo Ikulu
jijini Dar es salaam wakati alipokwenda kujitambulisha.
*****************************************************
Na Magreth Kinabo- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho wa mabalozi wawili wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
Utambulisho huo ulifanyika leo Ikulu jiji Dares Salaam, ambapo Balozi wa kwanza kuwakilisha hati ya utambulisho alikuwa ni Balozi wa India, Sandeep Arya na wa pili Balozi wa Denmark, Einer Jensen.
Akizungumza na Balozi wa Denrmak Jensen, Rais Kikwete aliomba aendelee kuendeleza ,ushirikaino wa baina ya nchi hizo katika maeneo mbalimbali.
“Kwa sasa tunatoa kipaumbele katika uwekezaji wa kibiashara, kwa kuwa ni eneo ambalo tunaweza kutengeneza ajira mpya pia tunaweza kuwasaidia watu kuweza kuondokana na umasikini,” alisema Rais.
Rais Kikwete aliyataja baadhi ya maeneo uwekezaji kuwa ni viwanda kutengenezea mbolea, madawa, na tunayo gesiasilia ya kutosha.

“Tunaweza kushirikiana katika maeneo mbalimbali. Hivyo hakuna kiongozi ambaye atakayeweza kusitisha ushirikiano wetu kwa kuwa ni agenda yetu hata nikiondoka madarakani,” alisisitiza Rais Kikwete.
Akizungumzia kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Rais Kikwete alisema mchakato wa kumtafuta mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) na urudishaji fomu ulikwenda vizuri, hivyo kampeni zitaanza wakati wowote kuanzia sasa.
Aliongeza kuwa ana matumaini kwamba kampeni za uchaguzi zitaendeshwa kwa usalama kwa kuzingatia uhuru na haki.
Rais Kikwete alisema changamoto iliyopo katika harakati za uchaguzi ni kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kupiga kura.
Kwa upande wake wa Balozi wa Denmark, Jensen, alisema ana matumani kuwa mchakato wa uchaguzi huo utamalizika kwa usalama.Pia ushirikiano wa baina ya nchi hizo utaendelea kuimarika.

No comments:
Post a Comment