Habari za Punde

*RAIS KIKWETE ASAINI MISWADA YA SHERIA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava
Rais Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene baada ya kuweka saini kuridhia  Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Katibu Mkuu Waziri wa Fedha Dkt. Servacius Likwelile baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  Profesa Sifuni Mchome baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Mheshimiwa George Simbachawene, Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Saada Mkuya, Waziri wa Fedha na Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa,  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi baada ya hafla ya kuweka saini na kuridhia miswada ya  Sheria ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Uwazi na Uwajibikaji, Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Masoko ya Bidhaa na Muswada wa Tume ya Walimu.
 *************************************
PICHA NA IKULUTHE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Agosti 4, 2015, ametia saini Miswada ya Sheria mitano hadharani ikiwa ni hatua yake ya mwisho kabisa kuridhia Miswada ya Sheria akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika sherehe iliyofanyika katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam,Rais Kikwete ameridhia Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Uwazi na Uwajibikaji, Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Masoko ya Bidhaa na Muswada wa Tume ya Walimu.

Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na mamia ya wageni waalikwa, mawaziri wanaohusika na sekta hizo, Mheshimiwa George Simbachawene ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Saada Mkuya ambaye ni Waziri wa Fedha na Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wametoa maelezo ya miswada hiyo mitano kabla haijaridhiwa na Rais Kikwete.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue pia wamehudhuria sherehe hizo ambazo vile vile zimehudhuriwa na mawaziri wa Serikali, mabalozi, wawakilishi wa taasisi zisizokuwa za Kiserikali (NGO’s)  na wadau wengine wa sekta ambazo Miswada yake imeridhiwa.

Hiyo ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria hadharani. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2009 wakati Rais Kikwete aliporidhia hadharani Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha katika Uchaguzi.

Aidha, hiio ni mara ya mwisho kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria nchini kabla ya kuondoka madarakani mwanzoni mwa Novemba, 2015. Rais tayari amelivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


4 Agosti, 2015

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.