Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwakabidhi Baadhi ya Maafisa Vijana
vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Ujasiriamali na ubunifu, wakati wa hafla ya
ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini
Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwakabidhi Baadhi ya Maafisa Vijana
vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Ujasiriamali na ubunifu, wakati wa hafla ya
ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini
Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwakabidhi Baadhi ya Maafisa Vijana
vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Ujasiriamali na ubunifu, wakati wa hafla ya
ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini
Arusha. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimueleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa Chuo
cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof.Bonard Mwape wakati
wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana
jijini Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga na Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof. Bonard Mwape wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Vijana na Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari na Chuo cha ESAMI. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
******************************************
Na Hassan Silayo-MAELEZO ARUSHA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania itaendelea kuweka mipango endelevu ya kuwasaidia vijana ili waweze
kujiajiri na kuajiri wengine.
Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga
wakati akifunga mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu yaliyotolewa kwa Maafisa
Vijana.
Sihaba alisema kuwa kundi la vijana
ni kundi kubwa lenye changamoto nyingi za kiuchumi na kijamii zinazopelekea
kupunguza ufanisi katika uzalishaji mali kuanzia ngazi ya familia na taifa kwa
ujumla
“Serikali inadhamira ya dhati ya
kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili
kuwafanya vijana waweze kujikimu kimaisha kwa kujiajiri au kuajiri wengine na
hii inatokana na serikali kutambua changamoto zinazowakabili vijana ikiwa ni
kundi muhimu katika jamii” Alisema Sihaba.
Aidha Sihaba aliwataka Maafisa Vijana
kutumia elimu na ujuzi walioupata katika mafunzo hayo katika kuisaidia serikali
kutimiza dhamira yake ya kuwainua vijana kiuchumi na kulifanya kundi hilo
kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali kwa manufaa yao na
Taifa kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha
Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof Bonard Mwape aliishukuru
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kuwapa nafasi ya kutoa
mafunzo hayo kwa Maafisa Vijana watakayo yatumia katika kuwabadilisha fikra
vijana na kuwafanya waweze kujiajiri kupitia ujasiriamali.
Prof. Mwape aliongeza kuwa huu ni
mwanzo wa mambo mazuri yanayokuja kwa ajili ya vijana na kwa ushirikiano na
Serikali kupitia Wizara watahakikisha vijana wanakuwa wanakuwa sehemu muhimu
katika jamii hasa katika shughuli za uzalishaji mali.
Akizungumzia kuhusu faida za mafunzo
hayo Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Arusha Bi. Hanifa Ramadhani alisema
kuwa watatumia mbinu walizojifunza katika mafunzo hayo ili kukidhi mahitaji ya
vijana na kuwawezesha kujiajiri kupitia ujasiriamali na kuwafanya kushiriki
katika shughuli za uzalishaji mali
Mafunzo hayo ya Ujasiriamali na
Ubunifu yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo na Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) kwa
lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri na kuajiri wengine.





No comments:
Post a Comment