Habari za Punde

*TIMU YA KAMATI YA AMANI YA VIONGOZI WA DINI MKOA WA DAR WAJIFUA KUWAKABILI WENZAO WA MKOA WA ARUSHA

 Kikosi cha timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa katika picha ya pamoja baada ya mazoezi yao yanayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki kati yao na timu ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa Arusha unaotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi huu. 

Mbali na mchezo huo pia timu hizo zinatarajia kufanya shughuli za Kijamii, ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa na Vituo vya Albino kwa lengo la kudumisha Amani na Mshikamano Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unaotarajia kufanyika Oktoba 25.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (katikati) akimramba chenga beki wa timu pinzani wakati wa mazoezi hayo, yaliyofanyika leo asubuhi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Katika mazoezi hayo timu ya Alhad ilishinda mabao 3-1, yaliyofungwa na Nahodha huyo Alhad na la kufutia machozi la wapinzani likifungwana Saleh.
 ''Tulia nikuvishe kajikanzu kidogo wewe'', ndivyo Sheikh Alhad anavyoonekana kusema huku akimvisha na kumvua kanzu mpinzani wake. wakati wa mazoezi.
 Anakwenda na mpira la la la laaaaaa, akituliza kumhadaa mpinzani wake hapa....
 Mafoto akimtoka beki mpinzani wake.....
Beki wakijiandaa kuondoa mpira wa hatari langoni kwake...

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.