Balozi Mdogo wa China nchini Tanzania anayeishi Zanzibar Xie Yunliang akitoa salamu zake kwa wananchi na Viongozi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi mpya wa Hospitali ya Abdalla Mzee inayojengwa na Kampuni kutoka China Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipoweka jiwe la msingi katika ziara ya kufungua miradi ya maendeleo
Baadhi ya wananchi wa Mji na Vitoji vya Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba wakiwa katika sherehe za Uwekaji wa jiwe la Msingi wa ujenzi mpya wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani inayojengwa na kampuni kutoka China jiwe hilo lililowekwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein jana
Waziri wa Afya Rashid Suleiman akisalimiana na Wananchi wakati wa Sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi mpya wa Hospitali ya Abdalla Mzee pia kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kutoa hutuba yake katikasherehe hiyo jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Wananchi jana wakati sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali mpya ya Abdalla Mzee iliyopo Mkoani Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba akiwa katika ziara ya Moahuo kufungua miradi ya maendeleo. Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment