Habari za Punde

*UZINDUZI WA MRADI WA MAJI NA KITUO CHA MAENDELEO YA VIJANA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Bavuai Migombani Mkoa wa Magharibi Unguja leo alipofika kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua  Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katika  Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Bavuai Migombani Mkoa wa Magharibi Unguja,(kutoka kushoto) Nd,Abdalla Suleiman  Mkuu wa Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni  Hmad Yusuf Masauni. KWA PICHA ZAIDI BOFYA READ MORE

Wafanyakazi wa Mamlaka ya maji ZAWA wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua bomba la maji ikiwa ni ishara ya kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katika viwanja vya Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja (katikati) Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni  Hamad Yusuf Masauni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtwisha ndoo ya maji Fathiya Khamis Husein (Suza)baada ya kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katika viwanja vya Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo wakati alipotembelea mabanda ya maeonesho ya kazi mbali mbali katika kituo cha Maendeleo ya Vijana Mwembe madema leo akiwa katika ziara ya kuzindua Mradi wa Maji na Kituo hicho katika Jimbo la Kikwajuni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON)Nd,Abdalla Suleiman  (kulia)wakati alipotembelea kituo hicho Mwembe Madema kuona maendeleoya kazi mbali mbali zinazofanywa na vijana wa Jimbo la Kikwajuni  sambamba na uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na Salama katika Jimbo hilo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheinalipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) huko Mwembe madema Jimbo la Kikwajuni leo. Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.