Habari za Punde

*MAMA SALMA AWAASA WANA LINDI

Na Magreth Kinabo –Maelezo,Lindi
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini  kuhakikisha kwamba wanapiga kura ya ndiyo kwa mgombea wa kiti cha urais,Dkt. John Magufuli , mgombea kiti cha Ubunge Hassan Kaunje na wagombea viti cha udiwani  ili waweze kupata maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Mama   Kikwete ,ambaye  pia  ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya     Taifa ya  Chama Cha Mapinduzi(NEC) wa Wilaya Lindi ,wakati wa uzinduzi  wa kampeni ya chama hicho ya wilaya hiyo ili  iliyoambatana na uzinduzi wa Ilani ya CCM kwa lengo la kuinadi  na kuwanadi wagombea hao iliyofanyika kwenye uwanja wa Fisi.

“Leo nimekuja kufanya kazi hii moja  ya kuhakikisha mgombea wa kiti cha urais,  anashinda akiwemo mgombea wa kiti cha ubunge na wagombea  wa viti  vya  udiwani,” alisema Mama Kikwete huku akiinadi picha ya mgombea wa kiti cha urais  na kumnadi mgombea wa kiti cha Ubunge  na wagombea viti vya udiwani katika kata mbalimbali kupitia chama hicho.

 Mama Kikwete  aliongeza kwamba  ikiwa kila mtu atatoka na kufanya kampeni ya nguvu jimbo hilo litapata kura ya ndiyo viti hivyo.
Alisema  wananchi hao endapo  watafanya hivyo ifikapo Oktoba 25, mwaka huu, watakuwa wamefanya kazi iliyokamilika na watapata maendeleo kwani amani inapatikana  mahali ambapo kuna maendeleo. Pia aliwataka wananchi hao kuhakikisha watunza kadi zao za kupigia kura, wasije wakapoteza nafasi hiyo muhimu.

Mama Kikwete aliwataka wananchi hao, kukipa chama hicho kura ya ndiyo kwa sababu kina ilani, ni chama makini  na kinafanya kazi kwa mipango.
Akizungumzia kuhusu ilani ya chama hicho,Mama Kikwete alisema,ina mambo makubwa manne, ambayo ni kuondoa umasikini, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, kuendeleza vita ya kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Katika uzinduzi huo, Mama Kikwete alimkabidhi  vitendea kazi mgombea wa kiti cha Ubunge  ,ambavyo  ni Katiba ya CCM na ilani hiyo ili  aweze kufanya kazi  huku akishangiliwa na mamia ya watu walijitokeza uwanjani hapo wengi wao wakiwa ni vijana.
Pia aliwapokea wanachama wapya  12 kutoka Chama Cha Wananchi(CUF) walioongozwa na Laibu Kais, ambaye alikabidhi kadi na bendera ya chama hicho  na kuahidi kupeperusha bendera ya CCM  kila kata.

Kaisi na  waliokuwa wagombea wenzake wa kiti cha Ubunge 10 wameungana ili kumwuunga mkono Kaunje, hatua ambayo ilipongenzwa na Mama Kikwete.
“ Kura zipotosha huwezi kuhama kwenda chama kingine, bali mnaungana na kuwa kitu kimoja ni maneno mazuri ya kuiga mfano,” alisisitiza Mama Kikwete.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Lindi, Mzee Ally Mtopa aliwakemea watu wanaosema kuwa chama hicho hakijafanya  maendeleo, ambapo  alisema mtu anayesema  hivyo, sawa na kumdharau baba yake aliyempeleka shule.
Na  Magreth Kinabo-Maelezo,Lindi
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi(NEC) kutoka Zanzibar mkoa wa Mjini, Hadija Hassan Aboud ametoa  changamoto kwa wananchi wa wilaya ya  Lindi   kuhakikisha kwamba wanajitokeza kupiga kura ifikapo Oktoba 25, mwaka huu.
Aidha mjumbe huyo pia ameupongeza  mkoa wa Lindi kwa hatua ya maendeleo iliyofikia ukulinganisha na kipindi cha miaka ya nyuma.
Kauli hiyo  imetolewa jana jioni na  Bi. Hadijah  wakati wa uzinduzi  wa kampeni ya chama hicho ya wilaya ya Lindi Mjini iliyoambatana na uzinduzi wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa lengo la kuinadi , kumnadi mgombea wa kiti cha Urais Dkt. John Magufuli  na Ubunge ,ikiwemo kuwanadi wagombea wa viti vya udiwani ,iliyofanyika kwenye uwanja wa Fisi.
“Ninawaomba mjitokeze kupiga kura siku ya kupiga kura, kwani ni siku muhimu, mgombea hawezi kushinda usipopiga kura.Kura moja inathamani. Sisi kwetu siku ya kupiga kura hakuna kulima hata mgonjwa… anachukuliwa ili aweze kupiga kura. Kura moja ni mali,” alisema Bi. Hadijah.
Bi . Hadijah  Aliongeza kwamba wajitokeze kukipigia kura chama hicho, ili nchi ya Tanzania iendelee kuwa na amani.
Mjumbe huyo alialikwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya  Chama Cha Mapinduzi(NEC) wa Wilaya ya Lindi ,  kwenye uzinduzi huo ,alisema Lindi anayoifahamu siyo aliyoikuta.
“Zamani ukitoka Dares Salaam saa 11:00 asubuhi  unafika Lindi saa 3:00 usiku  huku uso ukiwa na vumbi. Leo ukitoka Dar es Salaam  saa 11:00 asubuhi unafika Lindi saa 5:00 asubuhi bila uso kuwa na vumbi. Maendeleo yaliyoko Lindi ni mafanikio na matunda ya utekelezaji wa  Ilani ya CCM,” alisisitiza.
Bi. Hadijah  akizungumzia kuhusu Ilani ya CCM ya sasa alisema katika ukurasa wa 71 imeonyesha kwamba kiwanja cha ndege kitafanyiwa marekebisho na kujengwa upya na  kimepewa kipaumbele.
 Alifafanua kuwa katika ukurasa wa 115 hadi 118 imeonyesha kuwa shughuli za vijana,wanawake,wajasiriamali, wafanyabiashara wadogo na wakubwa wataendelezwa, afya pia imo, yakiwemo mambo mengi.
Hivyo aliwataka  wananchi  hao kuwachagua wagombea  hao ili chama hicho kiweze kupata ushindi wa Tsunami.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.