Habari za Punde

*UZINDUZI WA MNARA WA KUMBUKUMBU ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata Utepe kushiria Uzinduzi wa Mnara wa kumbukumbu ya miaka50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,sherehe za Uzinduzihuo ulifanyika leo katika viwanja vya Michenzani Mjini Unguja (katikati) Mke wa Rais Mama mwanamwema Shein na (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa ZSSF Abduwakil Haji Hafidh.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)  na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakipata maelezo kutoka kwa Mshauri wa Ujenzi wa Kampuni ya Habconsult Bw.Habid Nuryanayohusiana na Ramani ua Ujenzi wa Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya uzinduzi wa Mnara huo leo uliopo Michenzani Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)naMkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na viongozi wengine wakati walipotembelea sehemu za mnara wa kumbukumbu baada ya uzinduzi uliofanyika   leo katika viwanja vya Michenzani Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akiangalia darubini wakati alipopanda juuu kabisa ya Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50ya Mapinduzi ya zanzibar kuangalia Mji wote wa Unguja baada ya kuuzindua rasmi leo katika viwanja vya Michenzani Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa Mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Michenzani Mjini Zanzibar (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,na Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee(kulia). Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.