Na Mwandishi Maalum – Maelezo
Vyombo vya habari nchini vimepongezwa kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kutoa
taarifa kwa wananchi wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi wa
10 mwaka huu.
Pongezi
hizo zimetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akiongea na viongozi wa menejimenti
ya wizara na taasisi zake kwenye kikao cha kazi kilichofanyika jijini Dar es
Salaam.
Prof. Gabriel
alisema kipindi cha uchaguzi vyombo vya habari vilifaya kazi kubwa ya
kuwahabarisha wananchi habari za uchaguzi kwa kuzingatia weledi wa taaluma yao
na hivyo kuwawezesha wananchi kujua mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea
hapa nchini.
Katibu Mkuu huyo ambaye hicho kilikuwa ni
kikao chake cha kwanza tangu ateuliwe kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo mwishoni
mwa mwezi wa kumi aliahidi kuwatumikia na kuwaheshimu wafanyakazi wa wizara
yake huku akisimamia majukumu ya kazi kwa kufauata kanuni, taratibu na sheria
za utumishi wa Umma.
“Hiki
ni kikao chetu cha kujipanga kwa ajili ya kazi, ni vyema tukajipanga huku
tukijuwa matarajio ya Mhe.
Rais kwetu ni yapi, wananchi tunaowatumikia wanategemea kupata nini kutoka
kwetu na mimi kama Katibu
Mkuu natarajia kupata nini kutoka kwenu”, Prof. Gabriel alisema.
Akimkaribisha
Katibu Mkuu huyo kuongea na viongozi hao Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali watu Titus Mkapa alisema kikao hicho ni maalum kwa ajili ya wizara
kujadili utekelezaji wa mipango ya wizara kwa kasi.
Wakitoa
maoni yao kwa nyakati
tofauti viongozi hao waliiomba Serikali iangalie upya bajeti ya wizara hiyo
ambayo ni ndogo ili iweze kuongezwa na
kuwawezesha kufanya kazi
zao kwa ufaisi zaidi.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TasuBa) Michael Kadinde alisema chuo hicho kimekuwa kikizalisha ajira kwa
wanafunzi wanaosoma hapo mara baada ya kumaliza masomo yao lakini wanafunzi
wengi wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na ada.
“Kuna
baadhi ya wanafunzi wanajiunga na chuo hiki wakiwa na elimu ya darasa la saba,
na hivi sasa Serikali itaanza kutoa elimu bure kwa wanafunzi kwa darasa la
kwanza hadi kidato cha nne”.
“Ninaiomba
Serikali iweze kuwaangalia wanafunzi hawa wa darasa la saba ambao wanasoma
chuoni kwetu ili nao waweze kupata elimu bure sawa na wanafunzi wa Sekondari”,
alisisitiza Kadinde.
Kikao
hicho kimeitishwa kufuatia kikao cha Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na
Makatibu wakuu, manaibu makatibu wakuu na watendaji wakuu wa Serikali kilichofayika mwishoni mwa wiki
ambapo alieleza matarajio yake na matarajio ya wananchi katika uongozi wake.
Hivyo aliagiza kila sekta ikae na kujipanga kufanya kazi ili kukidhi matarajio
ya wananchi.
No comments:
Post a Comment