Mtaalamu Kutoka Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Anton Palangyo, akizungumza na Waheshimiwa Madiwani (hawapo pichani) kuhusiana na masuala ya Maadili ya Viongozi wakati wa mafunzo maalum yaliyofanyika leo Njombe. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe Ngd Gualbert Mbujilo akifuatiwa na Afisa Serikali za Mtaa Mkoa wa Njombe.
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Njombe wakiwa kwenye Mafunzo ya Uongozi kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe.
**************************************
Madiwani
wa Halmashauri ya Mji Njombe wamepatiwa mafunzo juu ya maswala ya Uongozi Bora
na Kupiga vita vitendo vya Rushwa pindi wanapokuwa kwenye majukumu yao ya
Uongozi.
Akifungua
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe,Mtaalamu kutoka
TAKUKURU Ndugu Charles Nakembetwa alianza kwa kuwaeleza maana nzima ya
Uongozi,kwamba Uongozi ni kujua Dhamana, Dira na Mustakabali wa jamii na baada
ya Kujua Dira ni jukumu la Kiongozi kukaa mbele na kuiongoza jamii.
Akizungumza
katika Mafunzo hayo,Mtaalamu huyo alisema kuwa Viongozi wengi wanageuza maana
ya uongozi na kuona kama uongozi ni
kutumikiwa,kuabudiwa na ndio maana matukio ya kuomba rushwa yanaripotiwa mara
kwa mara.
‘Viongozi
wengi hawawatembelei watu kwenye Maeneo yao na kuishi kwa kuwa mfano wa jamii
wanayoiongoza.Wengi wamekuwa ni Wabaguzi na Wamekosa uwajibikaji kitu ambacho
ni kinyume na dhana nzima ya Uongozi.’’Alisema Ndugu Charles Nakembetwa.
Vile
vile amewasisitiza Madiwani hao kuwa TAKUKURU ni chombo cha Kuelimisha na
Kuhamasisha Viongozi kushiriki kikamilifu juu ya upambanaji wa maswala ya
rushwa, na wasisite kuripoti taarifa zozote zile zinazohusiana na maswala ya
rushwa ndani ya Halmashauri.
Nae
Mtaalamu Kutoka Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Ndg. Anton Palangyoamewataka
Madiwani hao wafuate maadili ya Uongozi na kutambua kama watakayokuwa wanafanya
ni sahihi au sio Sahihi, na pindi wanapogundua kuwa sio sahihi wajisahihishe
ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Baadhi
wa Madiwani waliohudhuria mafunzo hayo wamesema kuwa, Mafunzo hayo yamewajengea
uwezo na kuwaongezea ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Mafunzo
hayo yameendeshwa na Mtaalamu kutoka TAKUKURU, Mtaalamu kutoka Tume ya Maadili
ya Viongozi wa Umma,Afisa Serikali za Mitaa Mkoa wa Njombe, Kaimu Mkurugenzi
Halmashauri ya Mji Njombe,na Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Imetolewa
na Afisa Habari,
Halmashauri
ya Mji Njombe.
No comments:
Post a Comment