Habari za Punde

*SIMBA, YANGA ZAAGA RASMI MASHINDANO YA MAPINDUZI

TIMU kongwe za Simba na Yanga za jijini Dar es Salaam, nazo jioni ya leo zimeungana na mwenzao Azam Fc, kuyaaga rasmi mashindano ya Kombe la Mapinduzi baada ya Simba kuchapwa na Mtibwa Suga bao 1-0 katika mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza uliopigwa jioni ya leo huku Yanga nao wakiondoshwa na URA ya Uganda katika mchezo wa Nusu Fainali ya pili katika Uwanja wa Aman mjini Unguja usiku huu.

Katika mchezo wa Yanga na URA, Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake Amis Tambwe katika dakika ya 13, lililodumu hadi dakika ya 76 kipindi cha pili, baada ya Peter Lwasa kuisawazishia  URA kufuatia makosa ya safu ya ulinzi ya Yanga.

Baada ya kumalizika kwa dakika 90 za mchezo huo timu hizo ziliingia katika zoezi la mikwaju ya penati na hatimaye URA kuibuka kidedea kwa jumla ya mikwaju 4-3, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Penalti za Yanga zilifungwa na Kevin Yondan, Deo Munishi ‘Dida’ na Simon Msuva huku Malimi Busungu na Geoffrey Mwashiuya wakikosa, wakati za URA zimefungwa na Deo Othieno, Said Kyeyune, Jimmy Kulaba na Brian Bwete, wakati Sam Sekito akikosa.

Tambwe alifunga bao hilo kwa kichwa akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa URA, Brian Bwete kufuatia mchomo wa winga Simon Msuva.

URA sasa watakutana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa fainali utakaopigwa siku ya Jumatano Uwanja wa Aman.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.