Habari za Punde

*WAZIRI NAPE AVIPONGEZA VYOMBO VYA HABARI KWA KUFANYAKAZI NZURI WAKATI WA UCHAGUZI

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiongea na wahariri wa Vyombo vya Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. Mhe Nape alivipongezav yombo vya Habari kwakufanya wajibu wao katika kipindi cha uchaguzi mkuu na kuwaahidi kuwa Serikali itakuwa karibu nao sana na kuhimiza kuwa serikali ya awamu ya Tano itatunga sharia nzuri itakayo rahisisha utekelezaji wa majukumu myao. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Bw.Absalom Kibanda.
  Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Jamhuri Media Ltd Bw. Deodatus Balile akichangia hoja katika kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Mhariri mkuu wa Gazeti la The Guardian Bw. Jesse Kwayu akichangia hoja wakati wakati wa kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe .Nape Nnauye. Bw Kwayu alimsihi Mhe Nape, kuzidi kuwa karibu na waandishi na pia zitungwe sharia zitakazowawezesha waandishi wa habari kupata habari kwa urahisi na kufanyak azi yao ya kuhabarisha jamii.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.