Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia)akizungumza na mshauri wa maendeleo ya kimataifa wa kampuni ya Uk
sport Bi.Clare Barell juu ya miradi mbalimbali ya maendeleo ya michezo na kumuomba mwakilishi huyo kuwekeza kupitia kampuni yao katika miundombinu ya michezo hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, akizungumza jambo na mshauri wa maendeleo ya kimataifa wa kampuni ya Uk
sport Bi. Clare Barell. Kampuni hiyo ni mshirika wa Tanzania katika maendeleo ya Michezo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshauri wa maendeleo ya kimataifa wa kampuni ya Uk sport Bi. Clare Barell (wa pili kushoto)alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam,leo. Wengine pichani ni Kaimu mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge (wa pili kulia).
No comments:
Post a Comment