Habari za Punde

*YANGA YAJIIMARISHA KILELENI,TAMBWE AMSHUSHA KIIZA MBIO ZA UFUNGAJI BORA

YANGA ya jijini Dar es Salaam, leo imewashushia mvua ya magoli wadogo zao African Sport ya Tanga katika mchezo uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Yanga wameibuka na mabao 5-0, na kuendelea kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania bara wakifikisha jumla ya Pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 21, huku Simba SC wakiwa na pointi 48 na mechi 21 pia, wakirudi katika nafasi ya pili na Azam FC wakibaki na pointi zao 47 huku wao wakiwa na mchezo mmoja mkononi na kubaki nafasi ya tatu.
Mabao ya Yanga yalianza kupatikana katika dakika ya 32 kupitia kwa beki wake Kelvin Yondani, aliyepiga shuti akimalizia kazi nzuri ya Haruna Niyonzima, Donald Ngoma akafunga bao lake la 13 katika Ligi Kuu msimu huu dakika ya 37 kwa shuti pia, akimalizia krosi ya beki wa kulia aliye katika kiwango kizuri hivi sasa, Juma Abdul.  Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Bao la tatu lilifungwa na Amissi Tambwe ambaye naye leo amerejea kileleni katika mbio za kuwania ufungaji bora akimuondoa Hamis Kiiza kwa kufunga bao lake la 16 msimu huu katika Ligi Kuu dakika ya 51 na kutupia bao la 17 dakika ya 72.

Mshambuliaji Matheo Anthony aliyetokea benchi kipindi cha pili akaifungia Yanga bao la nne dakika ya 58, akiunganisha krosi ya mchezaji mwenzake wa Zanzibar, beki Mwinyi Hajji Mngwali. 

Wafungaji wa mabao ya leo wa Yanga ni SC leo beki, Kevin Yondan na washambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma, Mrundi Amissi Tambwe na Mzanzibar Matheo Anthony.

Baada ya mchezo huo wa leo, Yanga inatarajiwa kuondoka keshokutwa kwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya wenyeji APR utakaopigwa siku ya Jumamosi.

KIKOSI CHA YANGA SC: Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Bossou/paul nonga dk77, Pato Ngonyani, Deus Kaseke/Salum Telela dk61, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Matheo Anthony dk57, Amissi Tambwe na Haruna Niyonzima. 

KIKOSI CHA AFRICAN SPORTS: Kabali Faraji, Mwaita Ngereza, Hamza Kassim/Khalfan Twenye dk61, Juma Shemvuni, Rahim Juma, Ally Ally, Hussein Issa, Pera Mavuo, Rajab Isihaka, James Mendi na Omari Issa/Mohammed Mtindi dk73.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.