Habari za Punde

*YANGA YAWACHEZESHA KWATA MAAFANDE WA APR KAMBINI KWAO


Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Yanga wameanza vyema mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga mabingwa wa Rwanda, APR mabao 2-1.
Katika  mchezo huo uliofanyika kwenye  uwanja wa Amahoro, Rwanda, APR, Yanga ilitawala kipindi chote cha kwanza na kuwafanya mashabiki wa APR ambao wengi wao walikuwa ni wanajeshi kukaa kimya.
Kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm alimpa  unahodha mchezaji wa zamani wa APR, Haruna Niyonzima, kitendo ambacho kiliwafanya mashabiki wa soka wa Rayon na klabu nyingine kuishangalia Yanga na kuonekana kama ipo uwanja wa nyumbani.
Yanga ilianza kwa kasi katika mchezo huo na kupata bao kwanza katika dakika ya 20 kupitia Juma  Abdul kwa mkwaju wa mita 25 baada ya mabeki wa APR kumfanyia faulo Amissi  Tambwe.  Mpira huo wa faulo uliachwa na Niyonzima na Thaban Kamusoko kabla ya Juma Abdul kufumua shuti kali na kumpita kipa maarufu wa APR, Oliver Kwizera.
Bao hilo liliwafanya wachezaji wa APR kuchanganyikiwa na kuifanya Yanga kucheza kama ipo uwanja wa nyumbani.  Hadi mapumziko, Yanga ilikuwa mbele kwa bao 1-0.
APR walianza kipindi cha pili kwa kasi na kulishambulia kama nyuki lango la Yanga,  lakini mabeki wakiongozwa na Kelvin Yondani, Vincent Bossou, Haji Mwinyi Mngwali,  Pato  Ngonyani kwa kushirikiana na kipa wao, Ali  Mustafa waliokoa  hatari zote.
Yanga ilionekana kucheza kwa malengo zaidi katika kipindi  hicho na kulinda zaidi eneo la kiungo chini ya wachezaji wake,  Thaban Kamusoko, Niyonzima na Deus Kaseke ambao waliwanyima  wachezaji wa APR kupanga mashambulizi.
Kocha wa Yanga alifanya mabadiliko kwa kumtoa Tambwe na nafasi yake kuchukuliwa na Simon Msuva ambaye aliongeza kasi ya mashambulizi katika mechi hiyo ambayo ilihudhuriwa na wanajeshi kibao.
Yanga ikizinduka na kuongeza bao la pili katika dakika ya 74 kupitia kwa Kamusoko baada ya kupiga pasi zaidi ya 20 kablaya kufunga. kukiwa kumesalia  dakika 7 mpira kumalizika, Niyonzima alitoka  na nafasi yake kuchukuliwa na Mbuyu Twite ambaye alihimarisha safu ya ulinzi.
Makosa yaliyofanywa na kipa Ali Mustafa dakika za nyongeza, ziliizawadia goli la kufuta machozi APR kupitia kwa Patrick Sibomana. Kwa ushindi huo, Yanga imejiweka  katika nafasi nzuri ya kusonga mbele na inahitaji sare ya aina yoyote ili kucheza mzunguko wa pili. Mechi ya marudiano itachezwa Machi 19 kwenye uwanja wa Taifa jijini.
Azam nao watashuka dimbani majira ya saa moja huko jijini Johanesburg kukipiga na Bidvest Wits Kombe la Shirikisho.


More
Referees: Bienvenu SINKO (CIV)  -  Mamadou Sherif BOGBE (CIV)  -  Kouame Gabriel KANGAH (CIV) | Stadium: Chedly Zouiten , Tunis (TUN)



More
Referees: TBD | Stadium: Estadio do Calulo , Calulo (ANG)





More
Referees: Jackson Pavaza (NAM)  -  Matheus KANYANGA (NAM)  -  Isaskar BOOIS (NAM) | Stadium: Lucas 'Masterpieces' Moripe Stadium , Pretoria (RSA)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.