Na Zainab Nyamka, Dar
BARAZA la wazee wa Yanga wameomba kupewa ufafanuzi na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) pamoja na Baraza la Michezo nchini (BMT) kuhusiana na matumizi ya kadi zitakazoruhusiwa kupiga kura siku ya uchaguzi, baada ya kutokea sintofahamu miongoni mwa wanachama. Hilo limekuja baada ya taarifa kutolewa kuwa kadi za zamani ndizo tu zitakazotumika kupiga kura siku ya uchaguzi wa Viongozi wa Klabu hiyo.
Katibu mkuu wa baraza hilo, Ibrahim Akilimali amesema wanataka ufafanuzi zaidi kutoka TFF, kwani tangu kuanza kwa mfumo wa kadi mpya za benki ya Posta wanachama wengi walibadilisha kadi zao na kuondoka kwenye mfumo huo wa zamani ambapo hadi sasa kadi hizo wanazitumia kwa miaka miwili sasa.
"Kutokana na tamko lao la kutumia kadi za zamani na kuwabagua wale wenye kadi mpya na kusema walio na kadi za zamani ndiyo wanahaki ya kupiga kura kiuhalisia inaweza kuleta mgogoro kwa wanachama,"amesema Akilimali. Kwahiyo tunaomba TFF na BMT kuweza kutoa tamko la kutumika kwa kadi zote mbili kwani hata katika uchaguzi wa mwaka 2006 zilitumika kadi mbili Yanga kampuni na Yanga Asili. alisema Akilimali
Pia, Baraza la wazee limeomba TFF na BMT kuipa ruhusa Sekretarieti ya Yanga kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama wenye Ajenda ya uchaguzi mkuu ili wanachama wapewe taarifa kuhusu uchaguzi, na katika mkutano huo sekretarieti iwaalike viongozi kutoka wizara husika, TFF, DRFA (chamacha mpira wa miguu mkoa wa Dar es salaam) na wadau wote ili kushuhudia maamuzi ya wanachama wa Yanga huku wakiomba busara itumike na kudumisha umoja, amani na utulivu uliopo ndani ya klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment