Habari za Punde

*MKUU WA WILAYA KINONDONI MH. HAPI ASHIRIKI ZOEZI LA KUFANYA USAFI NA WAKAZI WA KIMARA

 Mh DC Ally Salum Hapi wa Kinondoni Mapema leo asubuhi alishiriki zoezi la kufanya usafi na wakazi wa Kimara pamoja na Vikundi mbali mbali Vikiongozwa na HIDAYA FOUNDATION ambao walikutana kwa Pamoja katika hospitali ya Kimara na kuanzia hospitalini hapo kufanya usafi Hapo.
DC alifika nakufanya usafi kwa pamoja na wananchi na Vikundi Hivyo  zaidi ya 5 akishirikiana na Wananchi.
Kisha baada ya usafi Palikuwa na Matembezi kutoka Hospitalini hapi hadi Kituo cha cha daladala cha Suka na kuwahutubia wananchi.
Mh DC Amewaomba Wananchi hao kuendeleza zoezi hilo la kufanya usafi katikamitaa yao kwa kujitolea kwa lengo la kudumisha usafi wa mazingira.
''Usafi ni Jambo muhimu sana na Jambo hili si la Serikali kwani ukiumwa kipindupindu Ni wewe na Sio Serikali, hivyo Tujitahidi kutunza mazingira tunayoishi. Lakini pia tujitahidi kusaidia kwa Hali na mali kwa Jamii yetu kwa kutoa Misaada mbali mbali ya Kijamii ili kuisaidia Serikali.''
Alisema Mh DC Hapi.
Aidha wananchi wa Kimara wakisoma risala yao kwa mgeni ramsi, waliiomba Serikali kuwajengea Kituo cha Polisi kutokana na kuwa na matukio mengi ya Ujambazi katika maeneo hayo, Ambapo Mhe Dc aliwaahidi kuzishughulikia Changamoto hizo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.