Habari za Punde

*FULL MKANDA MTANANGE WA YANGA v/s AZAM JANA YANGA WAKIBEBA KOMBE LA SHIRIKISHO

 Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma (katikati) akichuana na beki wa Azam Fc, Abdallah Kheri, wakati wa mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga ilishinda mabao 3-1. Kulia ni Amis Tambwe akijiandaa kutoa msaada.
**************************************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Yanga wamezidi kung’ara katika medani ya soka Tanzania baada ya kutwaa taji la pili katika msimu wa ligi wa 2015 na 2016.
Yanga imefanikiwa kutwaa kombe la Shirikisho la Azam Sports baada ya kuifunga timu ya Azam FC mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Deus Kaseke (juu) akichuana na Farid Mussa.
***********************************
Ushindi huo mtamu umeiweka timu hiyo katika chati ya juu katika sola la Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kutokana na ukweli kuwa imekuwa timu pekee kupata mfanikio hayo kwa msimu huu.
Mbali ya kuwa na makombe mawili, Yanga pia ni wawakilishi pekee katika ukanda wan chi za Cecafa kuingia hatua ya makundi (Robo fainali) ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Kipa wa Azam Fc, Aishi Manula, akipangua moja ya mpira wa hatari uliopigwa langoni kwake na Simon Msuva.
*************************************
Ushindi huo umeifanya Yanga kupata jumla ya sh. 131 milioni. Pesa hiyo inatokana na zawadi ya Sh 50 milioni ya kutwaa kombe la Shirikisho na zawadi ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ya Sh 81 milioni.
Haikuwa kazi rahisi kwa Yanga kutwaa kombe la Shirikisho kutokana na upinzani mkali wa timu ya Azam katika mechi hiyo. Azam FC ilianza mechi hiyo kwa kasi na kulishambulia lango la Yanga kama  nyuki katika dakika za mwanzoni na kukosa nafasi mbili za wazi, kupitia John Bocco na Mudathiri Yahaya.
Vibweka vya mashabiki wa Yanga, mmoja wa mashabiki wa Yanga akionekana akiwa na Vyungu vinavyofuka moshi wa ubani akiwa jukwaani huku akitembea jukwaa zima wakati mechi ikiendelea.
*************************************
Yanga ilizinduka katika dakika ya 8 na mchezaji wake, Donald Ngoma alikosa bao a wazi baada ya kupiga shuti hafifu lililodakwa kirahisi na kipa bora wa mashindano hayo, Aishi Manula.
Amis Tambwe akishangilia moja kati ya mabao yake mawili hiyo jana.
**********************************
Makosa yaliyofanywa na beki chipukizi wa Azam FC, Gadiel Michael yaliipa Yanga bao la kungoza katika dakika ya 10 kupitia kwa Amissi Tambwe aliyefunga kwa kchwa kufuatia krosi ya mchezaji bora wa mechi hiyo, Juma Abdul.
 Beki wa Yanga, Juma Abdul, akiruka kukwepa kwanja la beki wa Azam Fc, Gadiel Michael.
*************************************************
Michael alishindwa kumzuia Abdul kupiga krosi hiyo na kumfiki Tambwe akiwa katikati ya mabeki wawili wa  Azam, Kheri Abdallah na  Erasto Nyoni.
Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko. Azam FC ilianza kipindi cha pili kwa kufanya mabadiliko kwa kumtoa Bocco  na nafasi yake kuchukuliwa na Didier Kavumbagu, mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya mchezo. Yanga ilifunga bao la pili kupitia kwa Tambwe katika dakika ya 47 baada ya kumzidi mbio Michael na kupiga krosi safi kwa Tambwe aliyefunga kirahisi.
Azam FC ilisawazisha dakika moja baadaye kupitia kwa Kavumbagu  baada ya kupokea pasi ya Ramadhan Singano. Bao la tatu la Yanga lilifungwa na Deus Kaseke kufuatia gonga safi za Thabani Kamusoko na Msuva ambaye alitengeneza mabao mawili katika mechi hiyo.
 Mchezaji wa Ndanda Fc, Atupele Green, akipokea zawadi ya mfungaji bora wa mashindano hayo.
*****************************************
Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikabidhi medali na kombe kwa washindi wa mechi hiyo pamoja na Atupele Green wa Ndanda FC aliyeibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao matano. Zawadi ya kipa Bora ilichukuliwa na Aishi Manula na mchezaji bora wa mechi ya fainali ni Juma Abdul.
 Beki wa Yanga Mwinyi Haji (kulia) akichuana na Ramadhan Singano.
 Mwinyi Haji,akimfinya Erasto Nyoni....
 Mwinyi Haji (kulia) akichuana kuwania mpira na Singano....
 Shabiki wa Yanga, akikatiza mitaa ya Keko huku akiwa amejichora mwilini wakati akielekea Uwanjani.
 Sehemu ya mashabiki wa Yanga.
 Msuava akiwania mpira na Agrey
 Ilikuwa ni mshike mshike.....
 Ngoma, akichuana na Morris
 Sehemu ya mashabiki wa Yanga.......
 Azam wakiwa Live kurusha mechi hiyo....
 Sehemu ya mashabiki wa Yanga, wakiwa jukwaani na mchezaji mpya wa Yanga,Hassan Kessy
 Msemaji wa Yanga, Jerry  Murro, akiwachangamsha mashabiki wake jukwaani
 Sehemu ya Mashabiki wa Yanga....
 Hassan Kessy, akiwa jukwaani akifuatilia mtanange huo....
 ''Nakuomba urudi timu ya Taifa'', Rais wa TFF,Jamal Malinzi akimnong'oneza beki wa Yanga Nadir Haroub 'Canavaro', wakati akisalimia benchi la Yanga.
 Wachezaji wa Yanga wakipokea zawadi zao
 Beki wa Yanga, Juma Abdul, akipokea zawadi yake ya kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
 Kipa wa Azam Fc, Aishi Manula, akipokea zawadi yake ya Kipa bora wa mechi.
 Juma Abdul. akipongezwa na Kocha wake baada ya kupokea zawadi.
 Juma Abdul, akisalimiana na Hassan Kessy na kumkaribisha rasmi kundini na kumtambulisha kwa mashabiki wa Yanga.
 Juma Abdul akizunguka na Hassan Kessy kumtambulisha kwa mashabiki....
 Karibu sana dogo.....
 Canavaro akisalimiana na kupeana fair play na Said Morad baada ya mchezo huo.
 Warembo wakiwasilisha zawadi uwanjani baada ya mchezo huo.
 Hassan Kessy, akijitambulisha kwa mashabiki wa Yanga huku akionyesha staili yake ya kupaa A.K.A Wa Kimataifa.
 Kaseke akimtoka Mugilaneza....
Kaseke (katikati) akiwatoka Singano (kulia) na Nyoni

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.