Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' akipokea Kombe la ubingwa wa Kombe la Azam Sports Federation, kutoka kwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi, baada ya kuwafunga Azam Fc katika mchezo wa Fainali uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Katika mchezo huo Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 3-1
**********************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
TIMU ya Yanga ya jijini Dar es
Salaam, baada ya kutwaa kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/ 2016,
hivi majuzi, leo tena wamedhihirisha ubora wao kwa kutwaa na Kombe la Azam
Sports Federation kwa kuwachapa Azam Fc mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jioni ya leo.
Kwa ushindi huo, sasa Yanga ni
mbabe asiyepingika wa soka ya Tanzania, baada ya awali kutwaa Ngao ya Jamii
Agosti 22, mwaka jana waliposhinda kwa penalti 8-7 dhidi ya Azam FC pia baada
ya sare ya 2-2 na Maji Maji mapema mwezi huu walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania
Bara.
Katika mchezo wa leo
uliochezeshwa na Mwamuzi Israel Nkongo, hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele
kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji kutoka Burundi, Amissi Tambwe katika dakika
ya tisa kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia, Juma Abdul.
Alikuwa ni Amis Tambwe tena akawafungia
Yanga bao la pili, safari hiyo akimalizia krosi ya winga Simon Msuva.
Na Azam walifanikiwa kupata bao
kupitia kwa Didier Kavumbagu katika dakika ya 48 baada ya kutengeneza nafasi
mbili nzuri, ambazo walishindwa kumalizia kuzitumia vizuri.
Kavumbagu alifunga bao hilo
baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Nahodha, John Raphael
Bocco.
Kiungo Deus Kaseke akaifungia
Yanga bao la tatu dakika ya 81 kwa mpira wa kupresi huku akimchambua kipa Aishi
Manula akimalizia pasi ya Msuva.
Canavaro, akipokea mfano wa hundi ya Sh. Milion 50 kutoka kwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi baada ya mchezo huo
Wachezaji wa Yanga, wakishangilia baada ya kupokea Kombe lao.
Baadhi ya wachezaji wa Azam Fc, wakipokea Medali zao.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia huku wakiwa na kombe lao.
KWA MATUKIO ZAIDI YA PICHA ZA MTANANGE HUU, NA HABARI KAMILI ZITAWAJIA HAPO BAADAYE, KAA NASI.





No comments:
Post a Comment