Rais wa Muungano wa Comoros Kanali Azali Assoumani Boinakheri (kulia) alipokuwa akiapishwa na Jaji wa Mahkama ya Katiba Loutfi Soulaimaine (wa tatu kushoto) katika uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro jana kufuatia ushindi alioupata baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika April 10 /2016 na uchaguzi wa marudio mei 11 mwaka huu.
Rais wa Muungano wa Comoros Kanali Azali Assoumani Boinakheri akiapishwa na Jaji wa Mahkama ya Katiba Loutfi Soulaimaine (hayupo pichani ) katika uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro kufuatia ushindi alioupata baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika April 10 /2016 na uchaguzi wa marudio mei 11 mwaka huu.
Rais wa Muungano wa Comoros Kanali Azali Assoumani Boinakheri (kulia) alipokuwa akiapishwa na Jaji wa Mahakama ya Katiba Loutfi Soulaimaine (wa pili kushoto) katika uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro.
Rais mstaafu wa Muungano wa Comoro Dkt.Ikulilou Dhoinine akimkabidhi Bendera ya Nchi kama ishara ya kumakabidhi madaraka Rais Mpya wa Nchi hiyo Kanali Azali Assoumani Boinakheri (kushoto) baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika April 10 /2016 na uchaguzi wa marudio mei 11 mwaka huu,sherehe ya kuapishwa Rais huyo ilifanyika jana katika Uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Muungano wa Comoro Kanali Azali Assoumani Boinakheri.
Sehemu ya wageni mbali mbali na Viongozi wa nchi ya Comoro wakiwa katika sherehe ya kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Kanali Azali Assoumani Boinakheri (kushoto) baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika April 10 /2016 na uchaguzi wa marudio mey 11 mwaka huu,sherehe ya kuapishwa Rais huyo ilifanyika jana katika Uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro.
Rais Mstaafu wa Muungano wa Comoro Mhe,Dkt.Ikililou Dhoinine (kulia) akiwa katikapicha na Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri mara baada ya kuapishwa.
Makamo wa Rais wa Muungano wa Comoro Mhe,Jafar Ahmada Sais wa kisiwa cha Ngazija akiapishwa na Jaji wa mahakama ya katiba ya Nchi hiyo Mhe,Loutfi Soulaimane (hayupo pichani ) wakati wa sherehe za kuapishwa Rais kanali Azali na makamo wake 3 iliyofanyika jana.
Rais Mstaafu wa Muungano wa Comoro Mhe,Dkt.Ikililou Dhoinine (kulia) akiwa na Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri (wa pili kulia) mara baada ya kuapishwa akiwa na Makamu wake wawili Mhe,Abdullah Said Sharman (kushoto) wa Kisiwa cha Mwali na Mhe,Mustarigan Aboud wa Kisiwa cha Anjouan (wa pili kushoto) Rais Mstaafu wa Muungano wa Comoro Mhe,Dkt.Ikililou Dhoinine (kulia) akiwa katikapicha na Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri mara baada ya kuapishwa.
Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri akitoa salamu kwa kikosi cha Bendera mara baada ya kuapishwa.
Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi Comoro mara baada ya kuapishwa.
Sehemu ya wageni mbali mbali na wananchi wa Comoro wakiwa katika sherehe ya kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Kanali Azali Assoumani Boinakheri (kushoto) baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika April 10 /2016 na uchaguzi wa marudio mey 11 mwaka huu,sherehe ya kuapishwa Rais huyo ilifanyika leo katika Uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro. Picha na Ikulu. Picha na Ikulu












No comments:
Post a Comment