
Na Zainab Nyamka,Dar
BAADA ya kuiongoza timu yake kutetea ubingwa wa ligi kuu,
fainali ya kombe la FA na kuingia hatua ya makundi nahodha wa timu ya Yanga,
Nadir Haroub 'Canavaro' amesema kuwa watahakikisha wanapigana kufa na kupona
kuweza kuisaidia timu yao kuingia hatua ya nusu fainali kwani kama watafanya
vizuri michezo mitatu ya mwanzo basi watakuwa wameweza kuvuka makundi.
Canavaro amesema mwaka huu wamekuwa na kikosi bora ambacho
kimekuwa kikifanya vizuri katika mechi zake na kuleta ushindani wa hali ya juu katika kila mechi wanayocheza na hicho kinakuwa ndiyo msingi mkubwa kwao wa kufanya vizuri zaidi.
"Tumeingia hatua ya makundi na tunajua ni moja ya hatua
ngumu sana tuliopo ila michezo mitatu ya mwanzo tukipata alama basi tutaingia
nusu fainali na hatimaye fainali kabisa na ikiwezekana tutaleta kombe
nchini,"alisema Canavaro.
Na katika kujiandaa zaidi kocha mkuu Hans Van De
Pluijm anajua ni wapi atapeleka kikosi kwa ajili ya maandalizi zaidi kwani Juni
17 tunaanza kucheza na Mo Bejala ya nchini Algeria na siku 10 baadae kutakuwa na
mechi nyingine dhidi ya TP Mazembe Jijini Dar es Salaam.
Kwa sasa wachezaji wote wanatakiwa kujiweka sawa na
kuweka akilini picha nzima ya mashindano yaliyokuwa mbele yao katika kipindi hiki kwani kufanya
vizuri kwao kutawatambulisha kimataiafa zaidi na kulitambulisha taifa. WAKATI HUO HUO
Nahodha huyo akinong'onezwa jambo na Rais wa TFF,Jamal Malinzi katika mechi ya Juzi kati ya Azam na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Eti, alikuwa kimbembeleza kurejea Kikosini na kujiunga na timu ya Taifa.
******************************
Timu ya Taifa imeondoka Alfajiri ya leo huku nahodha huyo wa
zamani Canavaro akishindwa kujumuika na kikosi hicho kinachonolewa na Charles
Boniface Mkwasa na kuendelea kuweka msimamo wake wa kutokuchezea timu ya taifa
kwani ameshaamua na tayari barua ipo TFF.
"Nimeshaweka msimamo wangu kuwa sitachezea tena timu
yaTaifa na ndio maana sijajiunga nao kuelekea Kenya kwa ajili ya mchezo wa
kirafiki dhidi ya Harambee Stars,"amesema Canavaro.
Toka kujiengua kwa Canavaro,Mkwasa anamuita kwa mara ya
kwanza baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mechi alizocheza
akitoka katika majeruahi yaliyomuweka nje kwa takribani miezi mitatu bila
kucheza.

No comments:
Post a Comment