Habari za Punde

*ZIARA YA MKUU WA MKOA WA DODOMA MHE JORDAN RUGIMBANA KUKAGUA MAENDELEO YA UTENGENEZAJI WA MADAWATI WILAYANI CHEMBA NA KONDOA

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyevaa sweta) akikagua maendeleo ya utengenezaji madawati kwenye karakana zinazotengeneza madawati  ya wilaya za chemba na kondoa, leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyevaa sweta) akikagua maendeleo ya utengenezaji madawati kwenye karakana zinazotengeneza madawati  ya wilaya za chemba na kondoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyevaa sweta) akikagua maendeleo ya utengenezaji madawati kwenye karakana zinazotengeneza madawati  ya wilaya za chemba na kondoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyevaa sweta) akikagua maendeleo ya utengenezaji madawati kwenye karakana zinazotengeneza madawati  ya wilaya za chemba na kondoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (wa pili kutoka kulia walio kalia dawati) akikagua ubora wa madawati yanayotengenezwa na wilaya ya Chemba kwa lengo la kutekeleza agizo la Mhe. Rais la kumaliza tatizo la uhaba wa madawati
Mafundi wakiendelea na kazi ya utengenezaji madawati ya Wilaya za Chemba na Kondoa kama walivyokutwa Mei 30, 2016 wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kukagua maendeleo ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kumaliza tatizo la uhaba wa madawati.
*********************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana Mei 30, 2016 amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya kazi ya utengenezaji madawati katika Wilaya za Chemba na Kondoa.
Katika ziara yake, Mheshimiwa Rugimbana ameonesha kuridhishwa na hatua ya utengenezaji madawati iliyofikiwa na Wilaya ya Chemba na jitihada alizoziona zimempa imani kuwa kufikia mwishoni mwa mwezi Juni, 2016 Chemba watakuwa wamekamilisha agizo la Mheshimiwa Rais Magufuli la kumaliza tatizo la madawati.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mheshimiwa Ramadhan Maneno alimweleza Mkuu wa Mkoa Dodoma kuwa Wilaya hiyo ina upungufu wa madawati 9,400 na hadi kufikia Mei 30, 2016 tayari Chemba walikuwa wamekamilisha utengenezaji wa madawati 5,000. Aidha,  tayari wameisha kusanya vifaa ambavyo ni mbao na bomba za chuma (Flat Bar Pipes) vinavyotosheleza kutengeneza madawati yaliyobakia na tayari vifaa hivyo vipo kwenye karakana inayotengeneza madawati ya chemba na kazi ya utengenezaji inaendelea.
“Pamoja na kuwepo kwa changamoto za kukatika kwa umeme mara kwa mara, Wilaya imefanya jitihada za kuongeza idadi ya mafundi ili washambulie kazi ya madawati yaliyobakia na kuhakikisha inakamilika kabla ya mwisho wa mwezi Juni” aliongeza Mhe. Maneno.
Kwa upande wa Wilaya ya Kondoa, Mheshimiwa Rugimbana amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo kuhakikisha kazi ya kutengeneza madawati inafanyika kwenye kituo kimoja na Wilaya kuongeza nguvu ya kazi kwa kuongeza idadi ya mafundi  na vifaa ikijumuisha mbao na bomba za chuma (Flat Bar Pipes).
Aidha, ametaka kazi hiyo ifanyike hadi siku za Jumamosi na Jumapili, pia vituo vya kutengenezea madawati viwekwe taa za umeme ili kazi ya utengenezaji ifanyike usiku na mchana kwa utaratibu utakaofaa.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mheshimiwa Shaban Kissu ameahidi kufikia Juni 15, 2016 Kondoa itakua inamalizia utengenezaji wa madawati yanayohitajika kwenye Wilaya hiyo kwani kwa sasa wamenunua mbao kwa bei nafuu kutoka Wilaya ya Chemba na Bomba za Chuma (Flat Bar Pipes) kutoka viwandani ambapo kwa pamoja vifaa hivyo vitatosha kutengenezea madawati yaliyobakia kulingana na mahitaji.
Taarifa ya Wilaya ya Kondoa imeonesha kuwepo kwa upungufu wa madawati 10,580 wakati yaliyokamilika kutengenezwa hadi sasa ni madawati 2,299 na yaliyo katika hatua za mwisho za matengenezo ni madawati 1,322.
Akihitimisha ziara yake ya ukaguzi, Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rugimbana amezitaka Wilaya za Dodoma kushirikiana ikiwa ni pamoja na zile Wilaya zenye misitu kuzisaidia mbao Wilaya ambazo zina uhaba wa misitu, Wilaya zilizofanikiwa utengenezaji wa madawati kama Chemba na Dodoma kuwapa uzoefu Wilaya zenye changamoto na kuahidi kuwa mwishoni mwa wiki atakamilisha kufanya ziara ya ukaguzi wa madawati kwenye Wilaya za Chamwino, Kongwa, Mpwapwa na Bahi.

Imetolewa na:
Idara ya Mawasiliano ya Serikali
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
DODOMA
Mei 31, 2016

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.