Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
KLABU ya Azam FC, wameanza mazoezi yao ya kujiandaa na msimu ujao wa ligu Kuu Tanzania
Bara (2016-17) ikiwa chini ya benchi jipya la ufundi linaloongozwa na makocha
kutoka nchini Hispania, Zeben Hernandez na Msaidizi wake Yeray Romero, Kocha
Mkuu wa Viungo Jonas Garcia na Msaidizi wake, Pablo Borges huku Kocha wa Makipa
akiwa ni Jose Garcia na Daktari wa timu, Sergio Perez, akitarajia kutua nchini
muda wowote kuanzia sasa.
Akizungumza na Mtandao huu, Mtendaji mkuu wa Azam Fc, Saad Kawemba, alisema kuwa kwa sasa wapo
kwenye mikakati ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kwa kusajili wanne wa
kimataifa baada ya Didier Kvaumbagu na Allan Wanga kuondoka.
‘’Zaidi pia tunahitaji golikipa wa kimataifa ambaye atasaidiana
na Aishi Manula na ambaye pia atakuwa
msaada kwetu katika michuano ya kimataifa na katika ligi msimu ujao ambao tunahitaji ubingwa na
hilo linawezekana kwani nia tunayo,
Tunahitaji kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na
hata katika ligi pia ndiyo maana tunataka kufanya usajili utakaokuwa na manufaa
kwetu na tumeonelea ni bora kutafuta kwanza golikipa wa kimataifa, beki wa kati
na washambuliaji wawili wa kimataifa ambao watachukua nafasi za Kavumbagu na
Allan Wanga,"amesema Kawemba.
Aidha Kawemba, alisema kuwa kwa sasa wameamua kupandisha
vijana wanne kutoka timu ya vijana pia na wamefanya mchanganuo wa vikosi ambapo
kwa sasa watakuwa na vikosi viwili kila kimoja kitakuwa na wachezaji 22.
Makocha hao wataongezewa nguvu na makocha wengine wazawa
waliokuwepo na kikosi hicho msimu uliopita kama Kocha Msaidizi Dennis Kitambi
na Idd Abubakar, aliyekuwa akiwafua makipa wa Azam FC.

No comments:
Post a Comment